Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025 ambao hujulikana kama ‘Form five selection’ ni tukio kubwa katika sekata ya elimu nchini Tanzania, ni utaratibu uliowekwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET). Mchakato huu unahusisha uchaguzi wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano na vyuo vya kati na vya ufundi kwa mwaka husika, ambapo kwa mwaka 2025, wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wanachaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kidato cha tano au vyuo vya elimu ya ufundi.Uteuzi huu unafanyika baada ya kufanya tathmini ya matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, mahitaji ya shule na vyuo, na mapendekezo ya wanafunzi wenyewe kama yalivyowasilishwa kupitia mfumo wa Selform.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa huwekwa wazi kupitia tovuti ya TAMISEMI pamoja na NACTVET. Katika Makala hii tumekuwekea maelezo ya kina kuhusu namna mchakato uchaguzi ulivyofanyika, jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa na Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato Cha Tano Na Vyuo husika.
Mchakato wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati (form five selection)
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025 unaratibiwa na TAMISEMI. Lengo ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wenye sifa wanapata nafasi za kujiunga na shule za sekondari za kidato cha tano na vyuo mbalimbali. Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano llinahusisha wanafunzi kutoka shule za serikali, zisizo za serikali, na watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mitihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi hupangwa katika shule za vipaji kama vile Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls. Wengine hupangwa katika shule za sekondari za kutwa za kidato cha tano, na wengine katika shule za bweni za kitaifa.
Mchakato wa uchaguzi unahusisha hatua mbalimbali, kuanzia uandikishaji wa wanafunzi, utoaji wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne mwaka 2024 kufanya mabadiliko ya machaguo yao ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Kozi za vyuo vya kati kupitia mfumo wa Selform hadi kupanga wanafunzi kwenye shule au kozi za vyuo vya kati na elimu ya ufundi. Mchakato ulianza baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Wanafunzi waliofanya vizuri hupangwa katika shule na vyuo kulingana na ufaulu wao na nafasi zilizopo. Majina ya wanafunzi waliochaguliwa yatatangazwa mara tu Baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi kupitia mfumo wa Selform.
TAMISEMI yatoa Fursa kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024 kubadili Tahasusi na Kozi
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, inahakikisha kwamba wanafunzi wanachaguliwa kwa haki na uwazi. Kwa hivyo, iwapo unajiuliza ni jinsi gani utaweza kuangalia majina ya waliochaguliwa na jinsi ya kuapata fomu za ya kujiunga endelea kusoma Makala hii kwa maelekezo ya kina.
1 Tarehe ya Ramsi ya Kutangazwa Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Tano
Unaweza kuwa unajiuliza Je, Ni lini Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano yatatangazwa? Kwa mwaka 2025, tarehe ya kutangazwa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano ni tukio linalosubiriwa kwa hamu. Katika mwaka uliopita, majina haya yalitangazwa rasmi tarehe 30.05.2024 na Waziri wa Nchi, Or-Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb).
Kwa kuzingatia mwenendo huo wa miaka iliyopita, Majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano yanatarajiwa kutangazwa mapema mwezi Mei 2025 ili kutoa nafasi kwa wanafunzi na familia kujipanga kwa maandalizi ya kuripoti katika shule husika au kujiunga na vyuo vya kati.
2 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati
Kila mwaka, wanafunzi na wazazi wanatafuta taarifa juu ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati. taarifa hizi zinapatikana kwa urahisi kupitia tovuti za serikali. Kwa kawaida, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga hupatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz.
Ikiwa wewe ni mmoja wa wanaosubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati mwaka 2025, hatua zifuatazo zitakusaidia kuona majina yako au ya mwanao kwa urahisi. Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeweka mfumo wa mtandaoni ambao unarahisisha kufikia orodha ya wanafunzi waliochaguliwa.
Hatua kwa Hatua Mchakato wa Kuangalia Majina ya Form five selection Kupitia Tovuti ya TAMISEMI:
- Fungua Tovuti Rasmi: Anza kwa kutembelea tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kubonyeza https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/.
- Chagua Linki ya Form Five First Selection, 2025: Mara baada ya kufungua tovuti, tafuta sehemu yenye kichwa kinachosomeka ‘Form Five First Selection, 2025’. Hii itakupeleka kwenye ukurasa wenye orodha ya wanafunzi waliochaguliwa.
- Chagua Orodha ya Mikoa: Katika ukurasa utaona orodha ya mikoa mbalimbali. Chagua mkoa uliosoma au unaohusiana na eneo lako.
- Chagua Halmashauri Husika: Baada ya kuchagua mkoa, utaona orodha ya halmashauri ndani ya mkoa huo. Chagua halmashauri ambapo shule yako inapatikana.
- Chagua Shule Uliyosoma: Katika hatua hii, utaona shule zilizopo ndani ya halmashauri husika. Chagua shule uliyosoma ili kujua kama umechaguliwa.
- Pata Orodha ya Wanafunzi: Baada ya kuchagua shule, utaweza kuona orodha ya wanafunzi kutoka shule hiyo. Orodha hii inaonyesha majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule au vyuo walivyopangiwa kujiunga.
- Pata Maelekezo ya Kujiunga: Mwisho, baada ya kuona jina lako au la mwanao, unaweza kupata maelekezo zaidi ya kujiunga kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa kwenye tovuti husika.
3 Jinsi Ya Kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 Kimkoa
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi unapangiliwa kimikoa. Hii inarahisisha upatikanaji wa matokeo na maelekezo kwa wanafunzi na wazazi. Orodha ya Majina ya waliochaguliwa kimikoa itatolewa ikiwa na viungo vya moja kwa moja wenda kwenye matokeo ya uchaguzi.
Kupitia Linki za Mikoa hii itakuwezesha kuona matokeo ya uchaguzi moja kwa moja na kwa urahisi zaidi.
4 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu ya Ufundi 2025
Baada ya kupata habari za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano au chuo cha elimu ya ufundi, hatua inayofuata ni kupakua na kufuata maelekezo ya kujiunga. Maelekezo haya yanahusisha taarifa muhimu zinazohusiana na jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya kuanza masomo, kuripoti shuleni au chuoni, na mahitaji yote muhimu unayopaswa nayo. ufuatao ni mwongozo wa jinsi unavyoweza kupata maelekezo Maelekezo ya Kujiunga na kidato cha tano na vyuo:
- Tembelea Tovuti Rasmi: Anza kwa kutembelea tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia kiungo https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/. Hii ni sehemu ambayo taarifa zote zinazohusu uchaguzi na maelekezo ya kujiunga zinapatikana.
- Chagua Orodha ya Mikoa: Unapofika kwenye ukurasa wa uchaguzi, chagua mkoa wako kutoka kwenye orodha inayoonekana. Hii itakupeleka kwenye orodha ya halmashauri ndani ya mkoa uliouchagua.
- Chagua Halmashauri na Shule: Baada ya kuchagua mkoa, chagua halmashauri yako, kisha chagua jina la shule au chuo ulichopangwa. Hii ni hatua muhimu ili kuhakikisha unapata maelekezo sahihi kulingana na shule au chuo ulichopangiwa.
- Bofya Jina la Shule/Chuo: Mara baada ya kuchagua shule au chuo, bofya kwenye jina la shule au chuo hicho ili kufungua maelekezo ya kujiunga. Maelekezo haya yanaweza kuwa katika muundo wa PDF au waraka mwingine wa kielektroniki.
- Pakua na Hifadhi Maelekezo Hayo: Baada ya kuona waraka wa maelekezo, pakua na uhifadhi kwenye kifaa chako ili uweze kuyasoma kwa wakati wako. Ni muhimu kusoma na kuelewa kila kipengele cha maelekezo haya ili kuhakikisha unajiandaa ipasavyo.
- Fanya maandalizi Kulingana na Maelekezo: Soma kwa umakini maelekezo yote; yatakupa mwongozo wa mahitaji yote muhimu kama vile vifaa vya shule, tarehe za kuripoti, ada (ikiwa ipo), na taratibu nyingine za kujiunga.
Ni muhimu kuhakikisha kwamba unafuata maelekezo hayo kwa ufasaha ili kuepuka changamoto wakati wa kuanza masomo. Tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI na NACTVET ni rasilimali muhimu katika mchakato huu, hivyo hakikisha unazitembelea mara kwa mara kwa habari na msaada zaidi. aidha, kwa maelekezo au ufafanuzi zaidi unaweza kutembelea katika Ofisi za Elimu za Mikoa na Halmashauri au unaweza kupiga simu kwenye namba ya Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Ofisi ya Raisi – TAMISEMI kwa namba za simu 026 160210 au 0735 160210 kwa msaada zaidi.
Namna ya kubadili machaguo ya vyuo vya kati