Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni nyaraka muhimu sana kwa kila Mtanzania. Kinatumika kama uthibitisho wa utambulisho wa mmoja kwa kuwa na taarifa zake za kibinafsi, ikiwemo jina, tarehe ya kuzaliwa, na picha. Kwa watu ambao bado hawajapata vitambulisho rasmi kutoka NIDA, wanaweza kupata nakala au copy ya kitambulisho hiki mtandaoni kupitia mfumo wa NIDA. Kitambulisho cha NIDA kina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku kwa sababu kinasaidia katika sehemu mbalimbali za maisha ya kila siku kama vile kupata huduma za umma, huduma za kibenki na masuala mbalimbali katika biashara.
Watu wengi wanatafuta kitambulisho cha NIDA kwa sababu kimekuwa kipimo cha msingi katika mitindo ya utambulisho wa raia Tanzania. Kwa kuzingatia umuhimu wa kitambulisho hiki, ni lazima kuwa na nakala yake kama sehemu ya usalama wa taarifa za mtu binafsi. Hii inasaidia pia kuondoa uwezekano wa udanganyifu au matumizi mbaya ya taarifa za watu.

1 Mahitaji Muhimu Kabla ya Kujiandikisha au Kufanya usajili mtandaoni
Kabla ya kuanza mchakato wa kujiandikisha mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, ni muhimu kuhakikisha unaviandaa na kuvichunguza vyema vielelezo vyote vinavyohitajika. Hapa kuna orodha ya mahitaji muhimu ambayo kila mwombaji anapaswa kuwa navyo kabla ya kuanza mchakato wa usajili:
- Cheti cha kuzaliwa cha mwombaji
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa / kiapo cha mzazi mmoja.
- Kama uraia wa mwombaji ni wakurithi: thibitisha kwa nakala ya cheti cha kuzaliwa au nakala ya kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.
- Kama uraia wa mwombaji ni wa kujiandikisha, thibitisha kwa nakala ya uraia wa kujiandikisha (Dossier Number) ya mwombaji.
Kwa kuhakikisha unakuwa na nyaraka hizi kabla ya kuanza mchakato wa kujiandikisha, utaweza kufanya mchakato huu kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi. Hii itasaidia kuepusha ucheleweshaji wowote katika kupata kitambulisho chako cha taifa kutoka NIDA.
2 Mambo Muhimu ya Kuzingatia Wakati wa Ujazaji Fomu
Wakati wa mchakato wa kujiandikisha mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA, kuna mambo kadhaa muhimu ambayo kila mwombaji anapaswa kuzingatia ili kuhakikisha usajili unakamilika kwa urahisi na ufanisi. Hapa chini ni masuala ya msingi ambayo yanapaswa kufuatiliwa:
- Mwombaji anatakiwa kuwa na anuani ya barua pepe ambayo ataitumia kujisajili na kupokea kiunga kitakachomuwezesha kukamilisha usajili wake.
- Mwombaji anatakiwa kuwa na nyaraka zisizopungua mbili zitakazotumika kuthibitisha utambulisho wake. Mfano wa nyaraka hizo ni; Cheti cha kuzaliwa n.k.
- Mwombaji anatakiwa kufanya “scanning” ya nyaraka zake na kuziweka katika muundo wa PDF (usiozidi kurasa moja kwa kila kiambatisho) au picha katika muundo wa JPG au PNG.
- Ni muhimu Mwombaji kujaza Namba yake ya simu ya mkononi.
- Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa endapo amezaliwa Mwaka 1980 na kuendelea. Aidha, endapo Mwombaji amezaliwa kabla ya mwaka 1980 anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa au “Affidavit”.
- Kwa Waombaji wenye majina mengine; ni vyema kuandika majina hayo ili endapo ikatokea uhitaji wa kurekebisha majina yake iwe rahisi kutambulika.
- Mwombaji anatakiwa kufahamu majina ya Baba na Mama yake mzazi.
- Mwombaji ambaye ana Namba za Utambulisho (NIN) za wazazi wake; anatakiwa kuweka viambata halisi (kwa wazazi waliokwishapata vitambulisho vya Taifa).
- Mwombaji anatakiwa kujua namba ya Nyumba, Mtaa na kata anayoishi.
- Kwa Watanzania walioko nje ya Nchi, wanatakiwa kupata uthibitisho wa ukaazi katika Nchi husika kutoka kwa Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ili kujaza sehemu ya makazi, Mtaa/Kata kwa usahihi.
- Endapo Mwombaji amepata vyeti vya Shule, Namba ya mlipa kodi (TIN) na Kadi ya mpiga kura; ni vyema kuambatanisha.
- Mwombaji anatakiwa kujaza Fomu kwa usahihi na kuhakikisha viambata vyake na taarifa alizo jaza katika mfumo hazikinzani na taarifa nyingine, kama vile taarifa za Shule au Biashara.
- Mwombaji anatakiwa kujaza taarifa zake kwa usahihi, na kuchapisha taarifa hizo katika fomu na kwenda kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa napoishi kwa ajili ya kugongewa Mhuri na Saini ya Mwenyekiti wa Mtaa wake.
- Mwombaji anatakiwa kufika katika Ofisi ya NIDA iliyoko kwenye Wilaya yake ya makazi akiwa na fomu iliyokamilika (Fomu iliyogongwa Mhuri na kuwekwa Saini ya Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa), pamoja na nakala ngumu za viambatisho vyake alivyopakia katika mfumo wakati wa usajili kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili.
- Kwa Mwombaji ambaye anahitaji kupata maelezo ya ziada; asisite kufika katika ofisi ya NIDA iliyopo karibu.
Kwa kuzingatia mambo haya muhimu, utakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa katika mchakato wa kujisajili mtandaoni na kupata kitambulisho chako cha nchi kupitia NIDA bila matatizo yoyote.
3 Mchakato wa Jinsi ya kupata copy ya kitambulisho cha Nida Mtandaoni
Kujisajili mtandaoni kwa ajili ya kitambulisho cha NIDA ni mchakato rahisi ambao unahitaji kufuatwa kwa uangalifu. Hapa kuna hatua za kina katika mchakato huu.
Hatua za Kujisajili Mtandaoni kwa ajili ya kupata Nakala ya Kitambulisho cha NIDA
Kujisajili mtandaoni kupitia Mfumo wa NIDA ni mchakato rahisi ambao unahitaji kufata hatua hizi:
- Tembelea Tovuti ya Mfumo wa NIDA: Tembelea NIDA Portal kwa ajili ya mchakato wa maombi ya kitambulisho cha Taifa.
- Fungua Akaunti: Bofya “Create Account” na jaza maelezo muhimu.
- Thibitisha Barua Pepe: Utapokea barua pepe ya uthibitisho, fuata maagizo ili kukamilisha ufunguzi wa akaunti.
- Jaza Fomu ya Maombi: Kwanza angalia maelezo kwa umakini.
- Tuma Maombi: Hakikisha umekamilisha viambatanisho vyako.
- Tembelea Ofisi ya NIDA: Chukua fomu iliyochapishwa na vielelezo vyako.
- Ufuatiliaji wa Maombi: Fuata maendeleo yako mtandaoni.
Ambatisha nyaraka zifuatazo, viambatisho hivi ni vya lazima:
i. Cheti cha kuzaliwa,
ii. Barua ya utambulisho wa makazi kutoka Serikali ya Mtaa unakoishi,
iii. Cheti cha kuzaliwa au Kitambulisho cha Taifa cha mzazi mmoja.
Ambatisha viambatisho vya ziada ulivyonavyo kati ya vifuatavyo:
i. Vyeti vya Masomo-Msingi,Sekondari,Chuo,
ii. Pasi ya kusafiria,
iii. Leseni ya udereva,
iv. Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN),
v. Kadi ya bima ya afya,
vi. Kitambulisho cha mzanzibar mkaazi
Wasilisha fomu yako ya maombi kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA wilaya unakoishi kwa ajili ya kuchukuliwa alama za kibaiolojia (kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole) ili kupisha hatua zinazofuata ziendelee.
Mavazi ya kuzingatia wakati wa Usajili: Ili picha ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa itoke katika ubora uliokusudiwa pindi unapowasilisha fomu ya maombi kwenye ubalozi husika kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, unashauriwa kutovaa nguo; nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki au nguo za kung’aa, jezi, nguo zenye nembo, michoro au maandishi, kofia aina yoyote na kutopaka hina viganjani ili alama za vidole zisomeke kirahisi,
Hatua mbalimbali za usajili na utambuzi wa watu:-
i. Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili,
ii. Uhakiki wa awali wa fomu za maombi,
iii. Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta,
iv. Kuthibitishaji taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta,
v. Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki,
vi. Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu,
vii. Uhakiki wa mwisho,
viii.Uchapishaji, uhakiki wa ubora na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

Jinsi ya kupata Nakala ya Kitambulisho cha NIDA
Baada ya maombi yako kupitishwa, unaweza kupakua nakala ya kitambulisho chako kupitia mfumo wa E-NIDA.
- Ingia kwenye Akaunti Yako: Fungua tovuti ya E-NIDA Login kupitia link https://eonline.nida.go.tz/ , bofya linki ya kuingia (Login), ingiza taarifa zako na bofya ingia.
- Nenda Sehemu ya Kitambulisho Changu: Baada ya kuingia kwenye kaunti yako ya Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa , nenda moja kwa moja kwenye sehemu Kitambulisho Changu ili kupakua/kudownload nakala ya kitambulisho chako cha NIDA.
- Bonyeza Pakua Nakala: Katika hatua hii, nakala ya kitambulisho chako itapakuliwa.
4 Umuhimu wa nakala au copy ya kitambulisho cha NIDA Mtandaoni
Kupata nakala au copy ya kitambulisho cha NIDA ni muhimu kwa watu ambao hawajapata vitambulisho rasmi.
- Itasaidia Katika Uhifadhi wa Taarifa: Kuwepo na nakala ya mtandaoni itakuwezesha kupata taarifa zako wakati wowote.
- Kuhifadhi Taarifa: Hii ni muhimu ili kuhakikisha hutapoteza kitambulisho chako cha awali.
- Urahisi katika Kupata Huduma mbalimbali za serikali: Kitambulisho hiki kinahitajika Katika huduma nyingi za kiserikali; hivyo nakala itarahisisha mchakato wa kupata huduma hizo.
Nzuri inasaidia
Ni jinsi gani naweza pata nakala ya kitambulisho changu kama nilijiandikisha zamani kabla ya huu mfumo wa kujiandikisha online