Namba ya Utambulisho ya Taifa (NIDA) ni sehemu muhimu ya utambulisho kwa kila Mtanzania. Inatoa njia ya kuaminika ya kuthibitisha utambulisho katika shughuli mbalimbali za kiserikali na za kiraia. Namba hii inahitajika wakati wa kusajili laini za simu, kufungua akaunti za benki, kupata huduma za afya, na hata kuomba ajira. Katika ulimwengu wa leo ambapo huduma nyingi zinaendeshwa kidijitali, uwezo wa kupata namba hii kwa njia rahisi na ya haraka ni jambo linalothaminiwa na wengi.
Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS kunaleta urahisi na ufanisi zaidi. Njia hii imekuwa mbadala wa mfumo wa zamani wa USSD na inatoa fursa kwa Watanzania kupata namba zao bila malipo yoyote. Katika makala hii, tutaelezea hatua kwa hatua jinsi ya kupata namba yako ya NIDA kwa SMS, umuhimu wake, na mambo ya kuzingatia ili kuhakikisha mchakato huu unakamilika kwa mafanikio.
Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA kwa Simu kwa Njia ya SMS
Kupata namba ya NIDA kwa njia ya SMS imekuwa suluhisho rahisi na nafuu kwa Watanzania wengi. Hatua hizi rahisi husadia kuwawezesha kupata namba zao kwa haraka bila kuhangaika.

Hatua za Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS
Fungua Ujumbe Mpya: fungua programu ya ujumbe kwenye simu yako.
Andika Ujumbe kwa kuFuata muundo huu: jina la kwanza*jina la mwisho*tarehe ya kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama
Kwa mfano: Juma*Mgeta*12031993*Asha*Mdoe. Hakikisha unaandika majina kwa herufi kubwa ili kuepuka makosa.
Tuma Ujumbe: Tuma ujumbe huo kwenda namba 15096. Huduma hii ni bure kabisa, hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu gharama.
Subiri Ujumbe wa Kujibu: Subiri ujumbe wa kujibu kutoka NIDA. Ujumbe huu utakuwa na namba yako ya NIDA. Hifadhi namba hii mahali salama kwani itakuhitajika mara kwa mara katika huduma mbalimbali.
Mambo ya Kuzingatia
Usahihi wa Taarifa: Hakikisha taarifa zote unazoandika ni sahihi kama zilivyojazwa kwenye fomu ya usajili wa NIDA. Taarifa zisizo sahihi zinaweza kusababisha kutokupata jibu sahihi.
Muundo wa Tarehe: Andika tarehe ya kuzaliwa kwa kufuata muundo huu: siku, mwezi, mwaka (DDMMYYYY).
Kama unakumbana na tatizo lolote katika kupata namba yako ya NIDA kwa njia ya SMS, unashauriwa kuangalia Namba yako ya NIDA kwa njia ya mtandao au unaweza kuomba msaada kupitia tovuti ya NIDA au kutembelea ofisi zao. Mfumo huu unaleta urahisi na uhalali wa kuthibitisha utambulisho wako unapohitaji huduma mbalimbali.
1 Umuhimu wa Namba ya NIDA au Kitambulisho cha NIDA
Namba ya Utambulisho ya Taifa (NIDA) na kitambulisho cha NIDA vina umuhimu mkubwa. Unaweza kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN)/Kitambulisho cha Taifa (NID) kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama:-
- Kusajili Laini ya Simu (Sim Card Registration),
- Kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN),
- Kusajili Biashara/Kampuni – BRELA,
- Kukata Hati ya Kusafiria ya Kielektroniki (E-Passport),
- Kukata Leseni ya Udereva,
- Kupata Huduma ya Afya,
- Kufungua Akaunti ya Benki,
- Kukopesheka Kirahisi kwenye Taasisi za Fedha,
- Kujiunga na Elimu Ngazi Mbalimbali,
- Kupata Mkopo wa Elimu ya Juu,
- Hati Miliki ya Kiwanja, Nyumba n.k,
- Kujidhamini na Kudhamini Wengine,
- Kitambulisho cha Taifa kutokana na kuwa na Kisilikoni (Cheap) kinaweza Kutumika kama Pochi ya Fedha ya Kielektroniki (E-Wallet) ambako unahifadhi fedha na kufanya malipo kwa kutumia Kitambulisho Chako,
- Kitambulisho kinaweza kutumika kama ATM CARD,
- Kwenye Maingio ya Malango Kielektroniki (E-Entrace),
- Daftari la Mahudhurio la Kielektroniki (Electronic Attendance),
- Mwananchi kuondokana na Adha ya Kubeba Utitiri wa Vitambulisho kwani sasa taarifa zote Muhimu za mwananchi zitapatikana katika Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu,
- Kinaweza kutumika kama hati ya Utambuzi wa Utaifa wa wananchi wanaovuka mipaka ndani ya nchi zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko,
- Vitaimarisha Utendaji Kazi Serikalini kwa Kuwa na Kumbukumbu Sahihi za Watumishi na Malipo ya Stahili zao, hasa Wanapostahafu,
- Kupata Ruzuku za Pembejeo za Kilimo Kirahisi,
- Kujisajili kwenye Chama cha Ushirika (Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Makundi mengine),
- Kupata Msaada wa TASAF unaotolewa kwa Kaya Masikini,
- Kufungua Akaunti ya Benki,
- Kuomba Ajira pamoja na Huduma Nyingine Nyingi.