Tumaini University Makumira (TUMA), iliyopo Arusha, ni moja ya vyuo vikuu maarufu nchini Tanzania. Chuo hiki kinatambulika kwa kutoa elimu bora inayochangia sana katika maendeleo ya elimu nchini. TUMA ilianza kama sehemu ya jitihada za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoa elimu yenye viwango vya juu na kutengeneza viongozi bora wa baadaye.
Sifa za Kujiunga Na Chuo Kikuu Cha Tumaini Makumira 2025/2026 ni mwongozo muhimu kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hiki. Ni muhimu kwani zinatoa mwanga juu ya vigezo vinavyohitajika ili kukidhi matakwa ya udahili, na hivyo kusaidia katika maandalizi ya wanafunzi.
Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Shahada ya Kwanza katika TUMA
Kwa mwanafunzi yeyote anayetaka kujiunga na programu za shahada ya kwanza katika Tumaini University Makumira, zifuatazo ni baadhi ya sifa zinazohitajika:
- Two principal passes katika masomo kama Historia, Jiografia, Kiswahili, au Lugha ya Kiingereza.
- Kiwango cha chini cha pointi 4.0 kinahitajika katika masomo yanayofafanua udahili kwenye programu husika.
Sifa na Vigezo vya Jumla kwa Kwa waombaji wa kidato cha sita (General Minimum Entry Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kabla ya 2014 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
2 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita mnamo 2014 na 2015 | Passi mbili kuu (‘C’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 kutoka kwa masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1; E = 0.5) |
3 | Waliohitimu Masomo ya Kidato cha Sita kuanzia 2016 | Passi mbili kuu (‘E’ na zaidi) zenye jumla ya alama 4.0 katika masomo mawili inayofafanua programu husika (ambapo A = 5; B = 4; C= 3; D = 2; E = 1; S = 0.5) |
Kwa waombaji wa Diploma (For Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications)
S/N | Aina ya Waombaji | Sifa za Kuingia |
1 | Waombaji wa Stashahada ya Kawaida, FTC na Sawa | Angalau pasi nne (“D” na zaidi) katika “O” Level au NVA Level III na chini ya pasi nne “O” Level au sawa na sifa za kigeni kama ilivyothibitishwa na NECTA au NACTVET; na i) Angalau GPA ya 3.0 kwa Stashahada ya Kawaida (NTA Level 6); au ii) Wastani wa alama “C” kwa Cheti cha Fundi Kamili (FTC) (ambapo A=5, B=4, C=3, na D=2); au iii) Wastani wa alama “B” kwa Stashahada ya Elimu ya Ualimu; au iv) Wastani wa alama “B” kwa tuzo zinazohusiana na Afya kama Tiba ya Kliniki na nyinginezo; au v) Alama ya Heshima kwa Stashahada na vyeti visivyofungamana na NTA; au vi) Upper Second Class kwa stashahada zisizo za NTA. |
2 | Cheti cha Msingi cha OUT | GPA ya 3.0 iliyokusanywa kutokana na masomo sita muhimu na angalau Alama ya “C” kutoka masomo matatu katika klusta husika (Sanaa, Sayansi na Masomo ya Biashara) pamoja na Cheti cha Juu cha Mtihani wa Elimu ya Sekondari kilicho na alama angalau 1.5 kutoka masomo mawili; au Stashahada ya Kawaida kutoka taasisi inayotambuliwa yenye GPA ya angalau 2.0 AU NTA level 5 / Cheti cha Fundi wa Kitaalam Kiwango cha II. |
Kwa orodha kamili ya programu na sifa za kujiunga, waombaji wanashauriwa kupakua Mwongozo wa Udahili wa TCU kupitia linki ifuatayo: TCU Guidebook.
Sifa za Jumla za Kujiunga na Programu za Uzamili na Uzamivu katika TUMA
Kwa waombaji wa programu za uzamili na uzamivu, mahitaji ni pamoja na:
- Shahada ya kwanza yenye GPA ya chini inayohitajika.
- Uzoefu wa kazi unahitajika kwa baadhi ya programu maalum.
- Mahitaji ya utafiti na machapisho kwa waombaji wa PhD.
Sifa na vigezo vya Kujiunga kwa Programu Zote
S/N | Kuingia katika | Sifa za Kuingia |
1 | Programu ya Cheti cha Uzamili | Angalau Shahada ya Kwanza (UQF level 8). |
2 | Programu ya Stashahada ya Uzamili | Cheti cha Uzamili AU Shahada ya Kwanza (UQF level 8) yenye GPA ya angalau 2.0 au alama ya C. |
3 | Programu ya Shahada ya Uzamili (aina zote) | a) Shahada ya Kwanza ya Kitaaluma inayofaa (UQF level 8) au sawa na hiyo yenye GPA ya 2.7 au alama ya B; b) Stashahada ya Uzamili katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B; au c) Sifa ya mafunzo ya kitaalam yenye mafunzo ya ziada yanayofaa, ushahidi wa uwezo wa utafiti na uzoefu wa kazi unaofaa. |
4 | Programu ya PhD (aina zote) | Shahada ya Uzamili (UQF level 9) katika fani/eneo husika au sawa na hiyo yenye GPA ya angalau 3.0 au alama ya B. |
Viwango hivi vinasaidia katika kuhakikisha kuwa wanafunzi ni wale wenye sifa na uwezo wa kufaulu katika programu hizi ngumu.
Makala hii imeangazia sifa muhimu za kujiunga na Tumaini University Makumira. Ushauri kwa waombaji ni kuanza mapema maandalizi yao, kuhakikisha wanakidhi vigezo vyote, na kuwa na nyaraka zote zinazohitajika wakati wa kuomba. Kwa habari zaidi, tembelea tovuti rasmi ya chuo au Wakala wa Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).