Table of Contents
1 Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Singida
Mkoa wa Singida unajulikana kwa kilimo na shughuli za biashara, pia umeweka mkazo mkubwa katika kuboresha sekta ya elimu. Walimu, wazazi, na jamii kwa ujumla wanatambua umuhimu wa elimu bora katika kuboresha maisha ya wanafunzi na jamii nzima. Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2024 yanatarajiwa kwa shauku kubwa na wanafunzi pamoja na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida. Makala hii itakusaidia kuelewa njia rahisi ya kuangalia matokeo ya darasa la saba kwa wanafunzi wa mkoa wa Singida.
2 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya la saba Mkoa wa Singida Kupitia Tovuti ya NECTA
Ili kuangalia matokeo ya darasa la saba kwa wanafunzi wa mkoa wa Singida, tumia tovuti ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa kufuata hatua hizi:
- Fungua kivinjari cha intaneti kupitia simu yako au kompyuta.
- Tembelea tovuti ya NECTA kwa kutembelea anwani ifuatayo: http://www.necta.go.tz.
- Ukishaingia, tafuta sehemu iliyoandikwa “Matokeo” kwenye ukurasa wa mwanzo.
- Bonyeza kwenye “Matokeo ya Darasa la Saba” lililopo kwenye orodha inayojitokeza.
- Bonyeza mwaka wa mtihani, yaani, “2024”.
- Tafuta mkoa wa Singida kupata matokeo.
- Tafuta jina la wilaya husika kupata matokeo.
- Tafuta jina mwanafunzi kupata matokeo.
- Matokeo yataonekana kwenye skrini, unaweza kuyaweka kama kumbukumbu au kuyachapisha kwa marejeo ya baadaye.
3 Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya zote za Mkoa wa Singida
Wilaya zote za mkoa wa Singida, zikiwemo Singida Mjini, Singida Vijijini, Iramba, Ikungi, Manyoni, na Mkalama, zinajitahidi kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu bora na matokeo yanayoakisi kazi kubwa wanayofanya. Kila wilaya inafanya kazi bega kwa bega na serikali na wadau wa elimu kuimarisha miundombinu ya shule na kutoa mafunzo endelevu kwa walimu ili kuboresha viwango vya elimu.
PSLE-2024 EXAMINATION RESULTS, MKOA WA SINGIDA
Ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao kipindi hiki muhimu cha maisha yao. Kuanzia hatua ya kufaulu mtihani wa darasa la saba hadi kujiunga na shule za sekondari, ni vyema kuwapa ushauri unaofaa na kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kusomea. Mafanikio haya ni mwanzo mpya kwa wanafunzi wa Singida na kuwasaidia kuelekea safari ya elimu ya sekondari itakayojenga msingi wa maisha yao ya baadaye.