Table of Contents
Mkoa wa Arusha, ukiwa moja ya mikoa maarufu nchini Tanzania, unatarajia kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwaka 2025. Uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza (Form One Selection) ni tukio linalosubiriwa kwa hamu na wanafunzi pamoja na wazazi wao. Uchaguzi huu unaratibiwa na TAMISEMI, na unahusisha wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali za mkoa wa Arusha ambao wamefanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2024. Katika makala hii, tutakupa mwongozo wa namna ya kuangalia matokeo ya uchaguzi huu pamoja na jinsi ya kupakua maelekezo ya kujiunga na shule sekondari kwa kidato cha kwanza.
Jinsi ya kuangalia Form One Selection Arusha
Kuangalia matokeo ya Form One Selection 2025 kwa mkoa wa Arusha ni rahisi na unaweza kufanywa kupitia mtandao. Fuata hatua zifuatazo ili uweze kuona kama mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza au la:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
- Nenda kwenye sehemu ya “Matangazo”.
- Bonyeza tangazo linalosema “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025”, ukurasa mpya utafunguaka na kisha chagua mkoa wa Arusha.
- Chagua Halmashauri
- Chagua Shule Uliyosoma
- Tafuta jina la mwanafunzi katika orodha iliyotolewa.
1 Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 Mkoa wa Rusha kiwilaya
Mkoa wa Arusha unajumuisha wilaya kadhaa, Kwa kawaida matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza yanapangwa kulingana na wilaya. Hii inaruhusu wazazi na wanafunzi kupata matokeo kwa urahisi zaidi. Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 kkwa Wilaya za Arusha ni kama zifuatazo:
Kuangalia kama mwanafunzi amechaguliwa tafadhali chchagua wilaya unayotaka kuona matokeo yake, Shule na tafuta jina la mwanafunzi.
Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 Arusha
Baada ya mwanafunzi kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga na shule aliyopangiwa. Maelekezo haya ni muhimu kwani yanaeleza mambo yote muhimu yanayohitajika kwa mwanafunzi kabla ya kuanza masomo. Ili kupakua maelekezo haya, fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.matokeo.necta.go.tz.
- Nenda kwenye sehemu ya “News”.
- Bofya linki ya “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025“.
- Tafuta jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi na kisha pakua maelekezo.
Kwa kufuata mwongozo huu, wazazi na wanafunzi wataweza kujua matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza kwa urahisi na kwa haraka, na pia kujiandaa vyema kwa ajili ya kuanza masomo mapya. Tunawatakia wanafunzi wote kila la heri katika safari yao ya elimu ya sekondari!