Table of Contents
Mkoa wa Manyara, unatarajia kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025. Hii ni hatua muhimu sana kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba 2024, kwani inaashiria mwanzo mpya wa safari ya kielimu katika ngazi ya sekondari. Uchaguzi huu unafanywa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Baraza La Mitihani La Taifa (NECTA) kwa kuzingatia vigezo kadhaa kama vile ufaulu wa wanafunzi na nafasi zilizopo katika shule za sekondari.
Jinsi ya kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 Mkoa wa Manyara
Kuna njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia ili kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025 katika mkoa wa Manyara. Njia kuu na rahisi ni kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI. Fuata hatua hizi kuhakikisha unapata matokeo kwa haraka:
- Tembelea tovuti ya TAMISEMI kwa anuani: www.tamisemi.go.tz
- Baada ya kufungua ukurasa wa mwanzo, Nenda kwenye sehemu ya “Matangazo”.
- Bonyeza tangazo linalosema “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025”,
- ukurasa mpya utafunguaka na kisha Chagua mkoa wa Manyara kutoka kwenye orodha ya mikoa.
- Chagua Halmashauri
- Chagua Shule Uliyosoma
- Baada ya kuchagua Shule, utaweza kuona orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na shule walizopangiwa.
- Tafuta jina la mwanafunzi katika orodha iliyotolewa.
Jinsi ya kuangalia Majina ya waliochaguliwa kidato cha kwanza Kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara
Mkoa wa Manyara una wilaya kadhaa, na unaweza kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kwa mgawanyo wa wilaya kama ifuatavyo:
1 Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 Manyara
Baada ya kuona majina ya wanafunzi waliochaguliwa, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga na shule husika. Maelekezo haya yanajumuisha taarifa muhimu kama vile vifaa vya shule vinavyohitajika na tarehe ya kuripoti. Ili kupakua maelekezo haya, fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.matokeo.necta.go.tz.
- Nenda kwenye sehemu ya “News”.
- Bofya linki ya “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025“.
- Tafuta jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi na kisha pakua maelekezo.
Kwa kufuata hatua hizi, utaweza kuhakikisha mwanafunzi wako anaandaliwa vizuri kwa ajili ya kuanza masomo ya sekondari mwaka 2025 katika mkoa wa Manyara.