Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imekamilisha Awamu ya pili ya udahili wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Katika awamu hii, waombaji wengi wamepata udahili katika vyuo mbalimbali, huku baadhi yao wakichaguliwa katika zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja. Hali hii inahitaji waombaji kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee ili kuruhusu mchakato wa udahili kuendelea kwa ufanisi. Kuangalia Majina ya Waombaji Waliodahiliwa Zaidi ya Chuo Kimoja au Programu Zaidi ya Moja katika Awamu ya Pili bofya linki hapo chini
Ni muhimu kwa waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja au programu zaidi ya moja kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee ndani ya muda uliopangwa. Pia, waombaji ambao hawakuthibitisha udahili wao katika Awamu ya Kwanza wanapaswa kutumia fursa ya Awamu ya Pili kuhakikisha wanapata nafasi ya kujiunga na programu za Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya TCU au wasiliana na vyuo husika.