Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imekamilisha Awamu ya Kwanza ya udahili wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Katika awamu hii, baadhi ya waombaji waliodahiliwa hawakuthibitisha udahili wao ndani ya muda uliopangwa, jambo ambalo linahitaji hatua za ziada ili kuhakikisha nafasi zao hazipotei.
Waombaji waliodahiliwa katika vyuo zaidi ya kimoja walitakiwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja pekee kuanzia tarehe 3 hadi 21 Septemba 2025. Uthibitisho huu ulifanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi (SMS) au barua pepe kwa waombaji.
Waombaji ambao hawakuthibitisha udahili wao ndani ya muda huu wapo katika hatari ya kupoteza nafasi zao za udahili kwani nafasi hizo zinaweza kutolewa kwa waombaji wengine katika Awamu ya Pili ya udahili.
Aidha, waombaji waliodahiliwa na chuo zaidi ya kimoja wanatakiwa kuthibitisha udahili wao ndani ya muda uliopangwa ili kuepuka kupoteza nafasi zao. Unaweza Kupata majina ya waombaji ambao hawakuthibitisha udahili wao katika Awamu ya Kwanza bofya linki hapo chini: