Katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi imetangaza orodha ya waombaji waliochaguliwa kushiriki katika usaili wa nafasi za usimamizi wa uchaguzi. Zoezi hili ni muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, uwazi, na haki.
Ratiba ya Usaili
Usaili utafanyika tarehe 15 oktoba 2025, katika katika Tarafa za Mwitikira (shule ya sekondari Mwitikira), Chipanga (shule ya Sekondari
Chipanga), Mundemu (shule ya Msingi Mundemu) na Bahi (shule ya Sekondari Bahi) kuanzia saa mbili kamili (2:00) asubuhi.. Waombaji wote walioteuliwa wanatakiwa kufika kwa wakati na kuzingatia maelekezo yaliyotolewa.
Orodha kamili ya waombaji waliochaguliwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya nafasi za kusimamia Uchaguzi Mkuu wa 2025 Wilaya ya Bahi inapatikana kwenye tovuti rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Waombaji wanashauriwa kupakua na kuchapisha orodha hiyo kwa marejeo yao.
KUITWA KWENYE USAILI WAOMBAJI WA TENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA UCHAGUZI MKUU WA 29 OKTABA,2025.