Table of Contents
Mtihani wa Kidato Cha Nne kwa mwaka 2025 ulifanyika kuanzia tarehe 17/11/2025hadi 28/11/2025 ambapo jumla ya wanafunzi 595,816 walifanya mtihani huo , watahiniwa 569,914 walikuwa ni wa shule na 25,902 walikuwa ni watahiniwa wa kujitegemea. Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) ni muhimu katika mfumo wa elimu ya Tanzania, kwani unatoa picha ya mafanikio ya wanafunzi katika miaka minne ya elimu ya sekondari. Mtihani huu, unasimamiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), unalenga kupima ufanisi wa wanafunzi katika masomo mbalimbali na kuamua hatima yao ya kitaaluma. Matokeo ya Kidato Cha Nne ni kipimo cha juhudi za wanafunzi na kielelezo cha ubora wa elimu katika shule na mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania. Mtihani huu ndio kipimo pekee ambacho huamua ikiwa mwanafunzi anastahili kuendelea katika masomo ya Kidato Cha Tano au kuelekea fursa nyingine za elimu ya vyuo vya kati.
1 Tarehe ya Kutangazwa kwa Matokeo ya Form four
Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) ni miongoni mwa taarifa muhimu zi nazowagusa wanafunzi, wazazi, na wadau wa elimu nchini Tanzania. Kwa kawaida, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hutangaza matokeo haya mwishoni mwa mwezi Januari kila mwaka. Kwa mfano, matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2024 yalitangazwa rasmi tarehe 23 Januari 2025. Kwa kuzingatia mwenendo huu, ni wazi kuwa matokeo ya Kidato Cha Nne 2025 yanatarajiwa kutangazwa rasmi na NECTA mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa tarehe hizi zinaweza kubadilika kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na changamoto za kiutawala au za kiufundi. Hivyo, ni muhimu kufuatilia tovuti rasmi ya NECTA kwa taarifa zaidi kuhusu tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya mwaka 2025.
2 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato Cha Nne, 2025 (Hatua kwa Hatua)
Mchakato wa Kupata matokeo yako ya Kidato Cha Nne (CSEE) 2025 mara baada ya kutangazwa na NECTA ni hatua muhimu sana ambayo kila mwanafunzi na mzazi anapaswa kuifahamu vizuri. Ili kuhakikisha unapata matokeo yako kwa haraka, kwa usahihi na kwa urahisi, hapa kuna mwongozo wa kina ambao unakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kuangalia matokeo yako mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya NECTA.
Kwa wanafunzi na wazazi wanaotaka kujua matokeo ya Kidato Cha Nne kwa mwaka 2025, wanaweza kufuata hatua zifuatazo:
Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA
Kwanza kabisa, unapaswa kuwa na kifaa cha kulichounganishwa na intaneti kama simu ya mkononi, kompyuta au tablet. Kisha, fungua kivinjari cha mtandao (browser) na andika anwani ya tovuti rasmi ya NECTA: https://necta.go.tz. Tovuti hii ndiyo chanzo rasmi cha matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Nne, hivyo hakikisha unatumia linki hii ili kuepuka taarifa zisizo rasmi au za uongo.
Tafuta Sehemu ya “News”
Baada ya kufungua tovuti ya NECTA, angalia kwenye ukurasa wa mbele kwa sehemu ya “News” au “Matangazo”. Hapa ndipo matangazo ya kawaida ya matokeo hutangazwa. Mara nyingi, linki ya matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Nne itaonekana pale kwa haraka mara tu matokeo yatakapotangazwa rasmi na NECTA.
Bofya Linki ya “MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2025 (Form four)”
Katika sehemu ya “News” utapata linki yenye maelezo kama “Matokeo ya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) 2025”. Bofya linki hiyo moja kwa moja kuingia kwenye ukurasa wa matokeo. Kupitia ukurasa wa matokeo utaweza kutafuta matokeo kwa jina la shule
Tafuta Jina la Shule
Katika ukurasa wa matokeo, utaona orodha ya shule zote zilizoshirki mtihani wa kidato cha nne 2025 ambapo utatakiwa kutafuta jina la shule yako. Tafuta jina la shule yako kutoka kwenye orodha na bonyeza kwenye linki ya shule hiyo ili kufungua matokeo ya shule.
Tafuta kwa Namba ya Mwanafunzi
Baada ya kuchagua jina la shule, sasa utaona orodha ya namba za wanafunzi na matokeo yao. Tafuta namba yako ya mtihani kwa makini ili kupata matokeo yako
Angalia Matokeo Yako
Mara utakapopata namba yako, angali matokeo yako kwa umakini . Matokeo yatakuonesha alama zako katika kila somo pamoja na alama ya jumla (Division).
Pakua au Chapisha Matokeo Yako
Baada ya kuona matokeo yako mtandaoni, unaweza kuchagua kupakua (download) au kuchapisha (print) matokeo hayo ili uwe nayo kwa uhifadhi. Ni muhimu kuhifadhi nakala ya matokeo yako kwa matumizi ya baadaye.
Kwa kufuata hatua hizi kwa umakini, utakuwa na uhakika wa kupata matokeo yako ya Kidato Cha Nne 2025 kwa haraka, salama na bila matatizo yoyote. Hii ni njia rahisi, ya kisasa na ya uhakika inayowezesha wanafunzi wote nchini Tanzania kufuatilia maendeleo yao ya kitaaluma.
3 Matokeo ya Kidato Cha Nne 2025 Kimkoa
Kwa wanafunzi wanaotaka kuona matokeo ya Kidato Cha Nne kwa mkoa wao, NECTA hutoa huduma ya kutafuta matokeo kwa mikoa na wilaya mbalimbali. Kuangalia matokeo ya kidatpo cha nne kimkoa unaweza kuchagua mkoa wako kutoka kwenye orodha ya mikoa hapo chini ili kuona matokeo ya shule na wanafunzi wa mkoa huo.
| ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
| GEITA | IRINGA | KAGERA |
| KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
| LINDI | MANYARA | MARA |
| MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
| MWANZA | NJOMBE | PWANI |
| RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
| SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
| TABORA | TANGA |

