Table of Contents
Wazazi, walezi, na wadau wa elimu katika Mkoa wa Dar es Salaam waamekuwa na hamu kubwa ya kujua matokeo ya mitihani ya darasa la nne. Matokeo haya yana umuhimu mkubwa kwani yanatoa tathmini ya maendeleo ya wanafunzi katika ngazi ya awali ya elimu ya msingi. Dar es Salaam, ikiwa ni kitovu cha kibiashara na makazi nchini Tanzania, ina idadi kubwa ya wanafunzi, na hivyo kufanya matokeo haya kuwa gumzo katika jamii.
Mkoa wa Dar es Salaam umejipatia umaarufu kutokana na shule zake zenye viwango bora vya elimu. Kutokana na uwepo wa shule za serikali na binafsi, wazazi wengi wanatarajia kuona watoto wao wakifanya vizuri katika mitihani hii. Matokeo mazuri kwa mwanafunzi ni chanzo cha furaha na ni hatua kubwa kuelekea elimu nzuri zaidi. Ikumbukwe kuwa, Dar es Salaam ina changamoto zake za kimasomo kama vile msongamano wa wanafunzi darasani, na matokeo haya pia yanatoa mwangaza juu ya namna ambavyo changamoto hizi zinaathiri elimu ya watoto.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya la nne Mkoa wa Dar es Salaam Kupitia Tovuti ya NECTA
Katika zama hizi za teknolojia, kufuatilia matokeo ya mitihani imekuwa rahisi na ya haraka zaidi kupitia mtandao. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewezesha watu kupata matokeo kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yao rasmi. Ili kuangalia matokeo ya darasa la nne kwa Mkoa wa Dar es Salaam, unahitaji kufanya yafuatayo:
- Tembelea Tovuti ya NECTA – Kwa kuanza, ingia kwenye kivinjari chako na uandike anwani ifuatayo: www.necta.go.tz. Hapo, utapata ukurasa wa nyumbani wa Baraza la Mitihani la Taifa.
- Chagua Kipengele cha Matokeo ya Darasa la Nne – Mara baada ya kufika kwenye tovuti, utaona orodha ya matokeo tofauti. Chagua “Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Nne” ili kufungua ukurasa wa matokeo hayo.
- Chagua Mkoa – Kutakuwa na orodha ya mikoa ambapo unaweza kuchagua mkoa wa “Dar es Salaam”
- Chagua Halmashauri Kutoka kwenye orodha ya Halmashauri zilizopo katika mkoa wa “Dar es Salaam”
- Tafuta Jina la shule ili kuPata Matokeo – Baada ya kuchagua Halmashauri, Utaona Orodha ya shule, Tafuta shule husika na bofya kwenye linki ya shule. Mara moja, matokeo ya shule yote yataonekana kwenye skrini yako.
- Tafuta Jina la mwanafunzi unayetaka kupata matokeo yake ili kuona matokeo.
Kwa wale ambao hawana uwezo wa kupata huduma za internet, wanaweza pia kutembelea shule husika ambapo matokeo hayo pia hubandikwa kwenye mbao za matangazo.
1 Matokeo ya Darasa la Nne Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam
Mkoa wa Dar es Salaam unaundwa na wilaya kadhaa ambazo ni Kinondoni, Ilala, na Temeke pamoja na wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni. Kila wilaya ina sifa za kipekee na changamoto zake katika elimu, lakini zote zina malengo sawa ya kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi. Unaweza kuona Matokeo ya Darasa la Nne Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam kupitia linki zifuatazo hapo chini