Matokeo ya darasa la nne ni mojawapo ya matokeo muhimu katika mfumo wa elimu wa Tanzania, yanayohusisha tathmini ya wanafunzi katika ngazi ya msingi. Mkoa wa Geita, ikiwa ni mojawapo ya mikoa mipya ambayo imeonyesha kujitahidi katika masuala ya elimu, unatoa matokeo haya kila mwaka kwa kufuata taratibu zinazowekwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Wazazi, walimu, na wanafunzi wana hamu kubwa ya kuona matokeo haya kwani ndiyo yanayotoa picha ya maendeleo ya kitaaluma katika Mkoa. Matokeo haya ni kipimo cha juhudi za walimu na wanafunzi pamoja na mwamko wa kielimu katika mkoa mzima.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne Mkoa wa Geita Kupitia Tovuti ya NECTA
Unaweza kuangalia matokeo ya darasa la nne kwa mwaka 2024/2025 katika mkoa wa Geita kwa kufuata hatua kadhaa kupitia tovuti rasmi ya NECTA.
- Kwanza, tembelea tovuti ya NECTA kwa kuandika anwani yake kwenye kivinjari chako: https://www.necta.go.tz/.
- Mara utakapokuwa kwenye tovuti hiyo, angalia sehemu ya ‘News’ ambayo mara nyingi hujumuisha viungo vya matokeo mbalimbali kila yanapotangazwa ikiwemo ya darasa la nne.
- Chagua linki ya matokeo MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024,
- Ukurasa wenye orodha ya mikoa utafunguka, chagua mkoa wa ‘Geita.’
- Bonyeza kwenye linki ya jina la mkoa ili kuonyesha matokeo ya wilaya zote.
- Ukurasa wenye orodha ya Halmashauri utafunguka, chagua Halmashauri au wialaya husika
- Tafuta Jina la shule kupata Matokeo ya shule husika
Matokeo ya Darasa la Nne Wilaya zote za Mkoa wa Geita
Mkoa wa Geita unajumuisha wilaya mbalimbali kama vile Geita Mjini, Chato, Nyang’hwale, Bukombe, na Mbogwe. Chagua Halmashauri yako ili kungalia Matokeo ya Darasa la Nne