“Holiday” ni wimbo mpya kutoka kwa msanii maarufu wa Bongo Flava, Diamond Platnumz. Wimbo huu ulitolewa rasmi tarehe 12 Oktoba 2024 kupitia Ziiki Media. Katika “Holiday”, Diamond Platnumz anachanganya midundo ya Amapiano na Bongo Flava, akielezea furaha na shauku ya kipindi cha mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Wimbo huu umeandaliwa na watayarishaji maarufu S2Kizzy na Sushi B kutoka Afrika Kusini. “Holiday” umevutia mashabiki wengi, na kufikia zaidi ya 1.8 milioni views kwenye YouTube ndani ya miezi minne tangu kutolewa kwake.
Kwa sasa, wimbo huu upo kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki mtandaoni, ikiwa ni pamoja na Apple Music.
Pakua wimbo huu na ufurahie midundo ya Diamond Platnumz katika “Holiday”.