Table of Contents
Mwaka 2025 umekuwa ni mwaka wa furaha kwa wanafunzi wengi ambao wamefaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2024 na kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza katika mkoa wa Dodoma. Uchaguzi huu ni hatua muhimu katika safari ya kielimu ya mwanafunzi hapa Tanzania. Mkoa wa Dodoma, kama ilivyo kwa mikoa mingine, unatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari. Katika makala hii, tutakuelekeza jinsi ya kutazama na kupakua matokeo ya uchaguzi wa Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2025 kwa mkoa wa Dodoma.
Jinsi ya kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 Mkoa wa Dodoma
Kutazama matokeo ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mkoani Dodoma ni mchakato rahisi ambao unaweza kufanyika mtandaoni. Fuata Hatua zifuatazi kuona jina la mwanafunzi
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
- Nenda kwenye sehemu ya “Matangazo”.
- Bonyeza tangazo linalosema “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025”,
- Ukurasa mpya utafunguaka na kisha Tafuta mkoa wa Dodoma bonyeza linki husika ili kupata orodha ya Halmashauri za Mkoa wa Dodoma
- Chagua Halmashauri Husika
- Chagua Shule Uliyosoma
- Tafuta jina la mwanafunzi katika orodha iliyotolewa.
1 Jinsi ya kuangalia Majina ya waliochaguliwa kidato cha kwanza Kwa wilaya zote za mkoa wa Dodoma
Mkoa wa Dodoma una wilaya kadhaa, Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa imetolewa kwa kila Wilaya. Ili kuona matokeo ya uchaguzi wa Kidato cha Kwanza kwa wilaya husika ndani ya Mkoa wa Dodoma, tumia linki zifuatazo:
2 Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 Dodoma
Baada ya kuona ni shule gani mwanafunzi amepangiwa, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga na shule hiyo. Hapa kuna jinsi ya kufanya hivyo:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.matokeo.necta.go.tz.
- Nenda kwenye sehemu ya “News”.
- Bofya linki ya “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025“.
- Tafuta jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi na kisha pakua maelekezo.
Kwa kufuata hatua hizi, utakuwa na uwezo wa kupata taarifa zote muhimu kuhusu uchaguzi wa Kidato cha Kwanza katika mkoa wa Dodoma kwa mwaka 2025. Tunawatakia wanafunzi wote kila la kheri katika safari yao mpya ya masomo!