Table of Contents
Kila mwaka, serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI hutoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kubadilisha machaguo yao ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Ualimu, Vyuo vya Kati na Elimu ya Ufundi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki. Mara tu baada ya mchakato wa uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali kukamilika TAMISEMI hutangaza majina rasmi ya wanafunzi waliochaguliwa.
Geita ni mkoa uliopo kaskazini magharibi mwa Tanzania. Wilaya ya Geita inajulikana kwa shughuli za uchimbaji madini, hasa dhahabu. Kigezo hiki kimetokea kutokana na idadi kubwa ya migodi inayopatikana humo. Katika uchaguzi huu wa Kidato cha Tano, wahitimu kutoka mkoa wa Geita wamepata fursa ya kujiunga na shule mbalimbali za sekondari na vyuo vya kati ili kujiendeleza kielimu.
Katika makala hii, tutajadili kwa kina kuhusu Jinsi ya kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano 2025 katika mkoa wa Geita na Jinsi ya kupakua fomu ya maelekezo.
1 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Kati, Katika Mkoa wa Geita
Kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati mwaka 2025 katika mkoa wa Geita ni rahisi na unapatikana kwa njia za kidijitali. Majina haya yanapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI na NACTVET. Unaweza kupitia hatua zifuatazo ili kuhakikisha unapata taarifa kamili:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI au NACTVET.
- Katika tovuti ya TAMISEMI, chagua kiunganishi cha “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025”.
- Fungua linki ya “Form Five First Selection, 2025”.
- Chagua orodha ya mikoa na kisha chagua mkoa wa Geita.
- Pata halmashauri husika ndani ya mkoa na chagua shule uliyosoma.
- Utapata orodha ya wanafunzi kutoka shule husika na maelekezo ya kujiunga.
2 Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 kwa Wialya za Mkoa wa Geita
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi unapangiliwa kiwilaya katika mkoa. Wanafunzi kutoka halmashauri tofauti katika mkoa wa Geita wamepangwa kwenye orodha ili kurahisisha kutambua majina ya waliochaguliwa.
CHAGUA HALMASHAURI
3 Jinsi Ya Kupata Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025
Baada ya kufahamu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano au chuo cha elimu ya ufundi, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga. Fuata maelekezo yafuatayo:
- Fungua tovuti ya TAMISEMI.
- Gusa linki ya jina la shule au chuo ulichopangiwa.
- Pakua maelekezo ya kujiunga na utayarishe mahitaji yote kabla ya kuanza masomo mapya.
Kwa kufuata hatua hizi na kuelewa mchakato, utaweza kuona majina ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano au Vyuo vya Elimu ya Ufundi mkoa wa Geita kwa urahisi.