Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano ni hatua muhimu inayofuata baada ya matokeo ya Kidato cha Nne kutangazwa. Kwa mwaka 2025, mchakato wa form five selection katika mkoa wa Kigoma unahusisha uteuzi wa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani yao ya Kidato cha Nne mwaka 2024. Huu ni mchakato wa kitaifa unaoendeshwa na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Katika mkoa wa Kigoma, uchaguzi huu huleta furaha na matumaini makubwa kwa wanafunzi na wazazi waliokwisha tarajia nafasi hii muhimu katika safari ya elimu ya juu zaidi.
Mchakato wa form five selection unahusisha mabadiliko ya machaguo ya Tahasusi (combinations) na programu mbalimbali zilizochaguliwa na wahitimu kabla ya kufanya mtihani wa Kidato cha Nne. Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki unaoitwa selform ambapo wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2024 waliweza kuomba kubadilisha machaguo yao ili kuhakikisha yanakidhi malengo yao ya kitaaluma. Kwa mwaka 2025, majina ya waliochaguliwa kidato cha tano katika Kigoma yatatangazwa baada ya kukamilika kwa mchakato huu wa uchaguzi.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo Vya Kati, Mkoa wa Kigoma
Kuhakikisha unapata taarifa sahihi za waliochaguliwa kidato cha tano mkoani Kigoma, ni muhimu kufuata mchakato rasmi. Kwa kawaida, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi inapatikana kwa njia ya mtandao kupitia tovuti rasmi za Ofisi ya Rais – TAMISEMI www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz. Pia, Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi unaopatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz utakuwa na taarifa hizi muhimu.
Ili kuona majina ya waliochaguliwa Fuata hatua hizi
- Tembelea Tovuti ya TAMISEMI: Fungua kivinjari chako na andika www.tamisemi.go.tz.
- Chagua Linki ya Uchaguzi: Tafuta na bonyeza kwenye linki iliyoandikwa “Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati 2025“
- Fungua Link ya Form Five First Selection, 2025: Kwenye ukurasa unaofunguka, bonyeza sehemu inayohusiana na form five selection 2025.
- Chagua Mkoa wa Kigoma: Kutoka kwenye orodha ya mikoa, tafuta na chagua Kigoma.
- Chagua Halmashauri na Shule: Baada ya kuchagua mkoa, endelea kuchagua halmashauri husika na shule uliyosoma kuangalia majina yaliyotoka.
- Angalia Orodha na Maelekezo: Utapata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kutoka shule husika pamoja na maelekezo ya kujiunga.
1 Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Kigoma
Unaweza kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa moja kwa moja kwa ngazi ya wilaya kupitia linki zifuatazo
- BUHIGWE DC
- KAKONKO DC
- KASULU DC
- KASULU TC
- KIBONDO DC
- KIGOMA DC
- KIGOMA UJIJI MC
- UVINZA DC
2 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Kigoma
Kupata maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Tano au chuo unachopaswa kufuata hatua rahisi. Tembelea tovuti ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz na fuata maelekezo yafuatayo:
- Fungua Tovuti ya TAMISEMI: Ingia kwenye tovuti kwa kutumia kiunganishi cha mtandao chako.
- Angalia Orodha ya Waliochaguliwa: Katika ukurasa wa mwanzo, pata kiunganishi kinachohusiana na waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo.
- Bofya Jina la Shule/Chuo: Mara baada ya kuona jina lako, bofya kwenye jina la shule/chuo kupata maelekezo rasmi ya kujiunga. Utapakua fomu husika na kupata maelekezo yanayoambatana nayo.
Kwa kuhitimisha, mchakato wa form five selection ni hatua muhimu katika kuendelea na elimu ya juu kwa wanafunzi wa mkoa wa Kigoma. Hakikisha unafuata taratibu zote zilizotolewa kupata matokeo yako kwa usahihi na kuendelea na hatua inayofuata katika safari yako ya kielimu.
3850