Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati mwaka 2025 ni hatua muhimu kwa wanafunzi wa mkoa wa Manyara. Mchakato huu wa form five selection ni sawa na safari inayojumuisha hatua mbalimbali, ambapo waliochaguliwa kidato cha tano wana nafasi ya kuendeleza elimu yao ngazi za juu. Mchakato huu ulihusisha hatua mbalimbali kuanzia kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne 2024 na wanafunzi waliofaulu mtihani wa Kidato cha Nne wa mwaka 2024,kupata fursa ya kubadili machaguo yao kupitia fumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) ambapo Matokeo ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo kwa mwaka 2025 yanatarajiwa kutangazwa mara tu baada ya mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kukamilika.Katika Makala hii tumekuwekea maelekezo kamili kuhusu jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati Katika Mkoa wa Manyara na jinsi ya kupakua maelekezo ya kujiunga
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati Mkoa wa Manyara
Kujua majina ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati mwaka 2025 ni rahisi kwa wanafunzi wa Manyara. Orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti rasmi za serikali kama TAMISEMI na NACTVET. Unaweza kuangalia majina hayo kwa kuingia kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI www.tamisemi.go.tz au Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz. Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) pia unapatikana kupitia kiunganishi selform.tamisemi.go.tz.
Hatua za kuangalia majina ni kama ifuatavyo:
- Tembelea tovuti ya www.tamisemi.go.tz au ingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi selform.tamisemi.go.tz.
- Bonyeza kiungo kinachosema “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025”.
- Chagua linki inayosema form five First Selection, 2025.
- Tafuta orodha ya mikoa na uchague Manyara.
- Tafuta halmashauri husika katika mkoa wa Manyara.
- Chagua shule uliyosoma kupata orodha ya wanafunzi kutoka shule husika.
- Fuata maelekezo ya kujiunga.
1 Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Manyara
Uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya kati unafanyika kwa kuzingatia wilaya na mikoa. Unaweza kupata orodha ya waliochaguliwa kidato cha tano kupitia linki za wilaya hapo chini
- BABATI DC
- BABATI TC
- HANANG DC
- KITETO DC
- MBULU DC
- MBULU TC
- SIMANJIRO DC
2 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Manyara
Kuapata maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati, tembelea tovuti TAMISEMI www.tamisemi.go.tz ili kuangalia kama umechaguliwa , baada ya kujua kama umechaguliwa . kuPakua maelekezo ya kujiunga kwa kubofya jina la shule ama chuo kilichochaguliwa.
Kwa wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano, mchakato huu utasaidia katika maandalizi ya safari mpya ya kielimu katika ngazi za juu ndani ya mkoa wa Manyara. Sasa unaweza kufurahia maendeleo yako ya kielimu ukijiwekea malengo zaidi katika masomo ya kidato cha tano na kozi za ufundi katikati ya mazingira mazuri ya mkoa huu.