Katika mkoa huu, kama ilivyo katika maeneo mengine ya nchi, uchaguzi huu ni nafasi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya Kidato cha Nne kupata nafasi za kujiendeleza kielimu kwa kujiunga na shule bora za sekondari za kidato cha tano na vyuo vya kati. Mkoa wa Mara upo kaskazini mwa Tanzania na unajulikana kwa vivutio kama vile Ziwa Victoria na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Mara ni moja ya mikoa inayochangia kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya elimu kwa kuwa na shule nyingi za sekondari, huku nyingi zikiwa zenye kutoa mafunzo bora na vipaji mbalimbali. Hii imefanya kuwa kitovu muhimu cha elimu, na kufanya majina ya waliochaguliwa kidato cha tano 2025 yasubiriwe kwa hamu kubwa sana na wazazi Pamoja na wanafunzi.
Kama ilivyo kwa mikoa mingine, Mchakato wa Form Five Selection katika mkoa wa Mara umeendeshwa kupitia mfumo wa kielektroniki ambapo wahitimu wa Kidato cha Nne walipata fursa ya kubadilisha machaguo yao ya Tahasusi za Kidato cha Tano na kozi za vyuo kupitia Fomu ya Uchaguzi (Selform). Mfumo huu uliratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na NACTVET, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanachaguliwa katika shule na vyuo wanavyovitaka kulingana na ufaulu wao.
Mwaka 2025, wahitimu wa Kidato cha Nne walitumia mfumo huu kubadili machaguo yao. Uchaguzi huu ulishirikisha wanafunzi wengi mkoani Mara, huku wengi wao wakitarajia kupangiwa kwenye shule za kidato cha tano na vyuo vya kati nchini.
1 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo Vya Kati katika Mkoa wa Mara
Kama unatafuta majina ya waliochaguliwa kidato cha tano 2025 katika mkoa wa Mara, unaweza kuyaangalia kwa kutumia Tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (www.nactvet.go.tz) au moja kwa moja kupitia Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Ili kupata majina haya, fuata hatua hizi: Kwanza, ingia kwenye tovuti ya TAMISEMI (selform.tamisemi.go.tz), kisha fungua linki ya “Selection results”. Baada ah apo, chagua orodha ya mkoa wa Mara, ikifuatiwa na kuchagua halmashauri husika. Hapo utaweza kupata orodha ya wanafunzi waliotoka kwenye shule mbalimbali na maelekezo ya kujiunga.
2 Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Mara
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka 2025 umepangiliwa kiwilaya na kimikoa. Mkoa wa Mara una wilaya zaidi ya sita ambazo zinashirikiana kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anayestahili ana nafasi ya kujiunga na shule anayoitaka.
CHAGUA HALMASHAURI
3 Jinsi Ya Kupata Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi mkoa wa Mara
Ili kufanikisha mchakato wa kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya elimu ya ufundi, unahitaji kupakua maelekezo ya kujiunga toka tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz). Hii ni pamoja na kuelewa kama umechaguliwa ama la.
Baada ya kufungua tovuti ya TAMISEM na kufanikiwa kuangalia jina lako, utabofya linki ya jina la shule au chuo ulichochaguliwa kujiunga nacho ili upate maelekezo husika ya kujiunga. Hii itakupa nafasi ya kujipanga na kujua nini kinachohitajika kabla ya kwenda kuanza masomo yako mapya.
Kwa ujumla, Form Five Selection 2025 kwa mkoa wa Mara ni hatua muhimu kwa wanafunzi na wazazi katika kupanga mipango ya masomo yao na kujiandaa kwa maisha ya baadaye katika elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi stadi.