Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati ni mchakato unaofanywa kila mwaka na Serikali ya Tanzania ili kuwaunganisha wanafunzi na masomo ya juu zaidi. Katika mkoa wa Morogoro, mchakato huu wa Form Five Selection 2025 ni muhimu kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2024. Kwa mwaka 2025, wanafunzi walipewa fursa ya kuchagua tahasusi mbalimbali na kozi mbalimbali za vyuo.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa ya kati nchini Tanzania. Morogoro ni mkoa unaofahamika kwa Kilimo na viwanda pamoja na wingi wa vyuo na shule za sekondari, jambo ambalo linaongeza umuhimu wa Form Five Selection katika kuhakikisha wanafunzi wanapata nafasi ya kuendeleza elimu yao.
Katika mwaka 2025, mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi katika mkoa wa Morogoro ulianza kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2024 kubadilisha machaguo yao kupitia mfumo wa selform. Mchakato huu ulihusisha fursa ya kubadilisha tahasusi na kozi mbalimbali kupitia Selform. Baada ya mchakato huo kukamilika, majina ya waliochaguliwa kidato cha tano katika mkoa wa Morogoro yatapatikana kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI na NACTVET
1 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Kati, katika Mkoa wa Morogoro
Ili kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati 2025 katika mkoa wa Morogoro, kuna hatua kadhaa unazopaswa kufuata. Kwa kawaida, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na fomu za kujiunga hutolewa kupitia tovuti rasmi kama Ofisi ya Rais TAMISEMI na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
- Tembelea Tovuti Rasmi: Ingia kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kutumia anwani www.tamisemi.go.tz au kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
- Chagua Kipengele cha Uchaguzi: Ukishafika kwenye tovuti, tafuta kipengele cha “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025” na bofya hapo.
- Fungua Linki ya Form Five First Selection, 2025: Chagua linki ya Form Five First Selection, 2025.
- Chagua Mkoa wa Morogoro: Kutoka kwenye orodha ya mikoa, chagua Morogoro ili kupata taarifa za mkoa huu pekee.
- Chagua Halmashauri na Shule: Utatakiwa kuchagua halmashauri kutoka katika mkoa na kisha kuchagua shule ambayo ulisoma ili kuona orodha ya wanafunzi waliochaguliwa.
Majina ya waliochaguliwa kidato cha tano yanatolewa kwa mpangilio wa shule na halmashauri, na maelekezo kuhusu jinsi ya kujiunga yanapatikana pia.
2 Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Morogoro
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi unapangiliwa kwa mfumo wa kiwilaya, unaowezesha kupata taarifa za kila wilaya ndani ya mkoa wa Morogoro. Hapa chini kuna mpangilio wa baadhi ya halmashauri zilizopo ndani ya mkoa:
- GAIRO DC
- IFAKARA TC
- KILOSA DC
- MALINYI DC
- MLIMBA DC
- MOROGORO DC
- MOROGORO MC
- MVOMERO DC
- ULANGA DC
Majina ya waliochaguliwa na maelekezo ya kujiunga yanapatikana kwa urahisi kwa kupitia linki ya halmashauri husika.
3 Jinsi Ya Kupata Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi Mkoa wa Morogoro
Kupata maelekezo ya kujiunga na kidato cha tano baada ya kuchaguliwa ni hatua muhimu ili kujiandaa na safari ya elimu ya juu. Ili kupakua maelekezo hayo:
- Fungua Tovuti ya TAMISEMI: Kwanza, hakikisha umeingia kwenye tovuti ya www.tamisemi.go.tz.
- Angalia Majina: Unatakiwa kujua kama umechaguliwa kwa kuperuzi majina yaliyotolewa kwenye tovuti.
- Bofya Jina la Shule/Chuo: Pale ambapo umekuta jina lako, bofya jina la shule au chuo ili uweze kuona na kupakua maelekezo ya kujiunga.
- Pakua na Kujaza Fomu: Pakua fomu za maelekezo na ujaze taarifa muhimu kama zitakavyohitajika.
Ni muhimu kufuata hatua hizi kwa makini ili kuhakikisha unajiandaa ipasavyo kwa masomo yako mapya. Katika mkoa wa Morogoro, uchaguzi wa waliochaguliwa kidato cha tano ni jambo la maana kwa maendeleo ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na wanayo matarajio ya elimu ya juu.