Table of Contents
Uchaguzi wa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati mwaka 2025, maarufu kama “Form Five Selection”, ni tukio muhimu kwa wanafunzi wa mkoa wa Mwanza. Mchakato huu unahusisha uchambuzi na uteuzi wa wanafunzi waliofaulu mitihani yao ya kidato cha nne, mwaka 2024, ili kujiunga na vyuo vya kati na kidato cha tano. Kwa wale waliochaguliwa kidato cha tano, hii ni hatua ya kwanza kuelekea kufanikisha ndoto zao za kitaaluma. Mchakato huu, unaendeshwa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kuanzia mchakato wa wanafunzi kuchagua tahasusi na kutoa orodha ya majina ya waliochaguliwa kidato cha tano.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati, katika Mkoa wa Mwanza
Kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati mwaka 2025 katika mkoa wa Mwanza, unapaswa kutembelea tovuti rasmi ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kupitia www.nactvet.go.tz. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa inapatikana kupitia Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Ili kuangalia majina hayo, tembelea tovuti ya TAMISEMI na elekeza kwenye sehemu ya Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati 2025. Fungua linki ya ‘Form Five First Selection, 2025’. Chagua orodha ya mikoa na teua Mwanza kutoka kwenye orodha hiyo. Chagua halmashauri yako kutoka kwenye orodha ya mikoa husika. Chagua shule uliyosoma ili kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa. Fuata maelekezo ya kujiunga yaliyotolewa.
1 Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi 2025 Kwa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi ambao unaendeshwa kitaifa, unakamilishwa kwa ngazi ya wilaya katika mkoa wa Mwanza. Kwa kubofya jina la halmashauri utapata moja kwa moja orodha ya waliochaguliwa kidato cha tano 2025 Mwanza.
- BUCHOSA DC
- ILEMELA MC
- KWIMBA DC
- MAGU DC
- MISUNGWI DC
- MWANZA CC
- SENGEREMA DC
- UKEREWE DC
2 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Mwanza
Kufuatia uteuzi wa waliochaguliwa kidato cha tano, ni muhimu kufahamu jinsi ya kupata maelekezo ya kujiunga. Tembelea tovuti ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz ili kuhakikisha kama umechaguliwa. Baada ya kufungua tovuti, fuata hatua hizi:
- Bofya linki ya jina la shule au chuo husika kujua kama umechaguliwa.
- Pakua fomu za maelekezo ya kujiunga kwa kubofya jina la shule/chuo.
Mchakato huu ni muhimu kwa kuhakikisha unafahamu ni nini kinachotakiwa katika hatua inayofuata baada ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano au chuo cha kati. Hakikisha unafuata maelekezo hayo kwa umakini ili kuongeza nafasi zako za kujiunga na taasisi husika.