Table of Contents
Mchakato wa Form Five Selection au Uchaguzi wa Wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati kwa mwaka 2025 katika mkoa wa Ruvuma ni zoezi muhimu linaloamua mustakabali wa elimu ya wahitimu wa Kidato cha Nne. Mchakato huu unahusisha kutathmini uwezo na sifa za wanafunzi waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2024 na kuwawezesha kujiunga na shule za sekondari za Kidato cha Tano au kuingia katika vyuo vya kati katika fursa mbalimbali za mafunzo. Wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 walishiriki katika mchakato wa kuchagua tahasusi za Kidato cha Tano na kozi mbalimbali za vyuo. Mchakato huu ulifanywa kupitia mfumo wa kielektroniki wa selform ambapo wanafunzi walibadilisha machaguo yao. Hatimaye, majina ya waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 katika mkoa wa Ruvuma yanatarajiwa kutangazwa kupitia tovuti ya TAMISEMI. Kupitia Makala hii utaweza kujua jinsi ya kuangalia majina hayo na kupakua fomu za kujiunga.
1 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo vya Kati katika Mkoa wa Ruvuma
Unaweza kuona majina ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 katika Ruvuma kupitia tovuti rasmi za serikali. Kawaida, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga zinapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz , Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz na Mfumo wa Student Selection MIS ambao unapatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Ili kuangalia majina hayo, fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti ya TAMISEMI kwenye kiunganishi hiki: UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI.
- Fungua linki ya Form Five First Selection, 2025.
- Chagua orodha ya mikoa na uchague Ruvuma.
- Kisha, chagua halmashauri husika.
- Chagua shule uliyohitimu.
- Pata orodha ya wanafunzi walioteuliwa kutoka shule hiyo na fuata maelekezo ya kujiunga.
2 Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za Mkoa wa Ruvuma
Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi Mwaka 2025, umepangiliwa kwa utaratibu wa wilaya katika mkoa wa Ruvuma. Hii inasaidia kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyefaulu anapewa fursa anayostahili.
Kuona matokeo ya uchaguzi moja kwa moja na kwa urahisi tumia linki zifuatazo.
CHAGUA HALMASHAURI
3 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Ruvuma
Unaweza kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Ruvuma kwa ku Tembelea Tovuti ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz. Hakiki kama umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi. Bofya jina la shule/chuo ili kupakua maelekezo ya kujiunga.
Kupitia hatua hizi, utapata mwongozo wa namna ya kujiunga na taasisi yako mpya ya elimu kwa mwaka 2025. Furaha na kheri njema kwa wale waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025 Ruvuma!