Form Five Selection ni mchakato muhimu katika mfumo wa elimu nchini Tanzania, ambapo wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne huchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati. Mchakato wa uchaguzi huu kwa wanafunzi wa Shinyanga unalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye sifa na waliofanya vyema katika mitihani yao ya Kidato cha Nne wanapata nafasi ya kuendelea na masomo ya juu. Uchaguzi huu unafanyika kwa kutumia mfumo wa kielektroniki unaosimamiwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI. Mchakato wa uchaguzi ni mwendelezo baada ya wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 kufanya mabadiliko ya machaguo ya tahasusi na kozi ambazo wangependa kusomea. Mfumo wa Selform uliwawezesha wanafunzi kubadilisha machaguo yao kabla ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati kutangazwa.
Jinsi ya kuangalia Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, katika mkoa wa Shinyanga
Kwa wale wanaosubiria kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo, ni muhimu kufahamu jinsi ya kuangalia ikiwa umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano au vyuo vya kati mwaka 2025 katika mkoa wa Shinyanga. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na fomu za kujiunga hupatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz). Vilevile, taarifa zinaweza kupatikana kupitia mfumo wa kielektroniki wa selform
Ili kuangalia majina ya waliochaguliwa, unahitaji kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti ya www.tamisemi.go.tz.
- Tafuta na fungua sehemu ya “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025”.
- Chagua linki ya “Form Five First Selection, 2025”.
- Kutoka hapa, chagua mkoa wa Shinyanga na halmashauri ambayo shule yako ipo.
- Chagua shule uliyosoma.
- Angalia orodha ya wanafunzi kutoka shule husika na Pakua maelekezo ya kujiunga.
Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 kwa Wilaya za mkoa wa Shinyanga
Kwa Shinyanga, mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi unafanyika kwa kupangwa kimkoa na kiwilaya, ambapo kila halmashauri ina linki maalum ya uchaguzi wa wanafunzi wake. Chagua jina la Halmashauri yako kupata orodha ya form five selection kwa mwaka 2025
CHAGUA HALMASHAURI
Jinsi Ya Kupata Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi mkoa wa Shinyanga
Kupata maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Tano au vyuo vya elimu ya ufundi ni muhimu kwa wanafunzi waliochaguliwa tembelea tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) na kuthibitisha kama umechaguliwa.
Ili kupakua maelekezo, unahitaji:
- Nenda kwenye tovuti ya www.tamisemi.go.tz.
- Tafuta sehemu iliyotajwa kwa ajili ya waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati.
- Bofya linki ya jina la shule au chuo unachotakiwa kujiunga ili kupakua maelekezo husika.
- Soma kwa makini maelekezo na uandae mahitaji yaliyoorodheshwa kabla ya tarehe ya kujiunga.
Kwa kuzingatia maelekezo haya, utaweza kujiandaa kikamilifu kwa hatua yako mpya ya kielimu. Ni matumaini yangu kuwa waliochaguliwa kidato cha tano mwaka 2025 mkoa wa Shinyanga watajiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya kati pasipo vikwazo, na kwamba mchakato wote utakua wa mafanikio kwa wote.