Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano au Form Five Selection ni tukio la kila mwaka ambalo huambatana na matarajio makubwa kwa wanafunzi na wazazi. Katika Mkoa wa Songwe, uchaguzi huu unajumuisha mchakato wa kuwachagua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2024 na kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha divisheni I hadi III ili kuendelea na mchakato wa elimu ya sekondari ya juu au vyuo vya kati.
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati mwaka 2025 katika Mkoa wa Songwe ulifanywa kupitia mfumo wa kielektroniki maarufu kama Selform. Mfumo huu uliwawezesha wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 kufanya mabadiliko ya machaguo mengine ya Tahasusi, Vyuo vya Ualimu, vyuo vya kati, na elimu ya ufundi. Baada ya kukamilisha mchakato huu, majina ya waliochaguliwa kuendelea na masomo Yatatangazwa kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI.
1 Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Kati, Katika Mkoa wa Songwe
Maendeleo ya dijitali yamekuwa chachu muhimu ya kupatikanaji wa taarifa muhimu kama majina ya waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ya juu na vyuo vya kati katika Mkoa wa Songwe. Orodha ya majina au Form Five Selection yanaweza kupatikana kwa urahisi kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI.
Ili kuangalia Majina ya waliochaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha tano mwaka 2025 utatakiwa kuingia kwenye tovuti kuu ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz
Ili kuangalia majina yako, kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI kwa linki hii: selform.tamisemi.go.tz.
- Chagua linki ya “Form Five First Selection 2025”.
- Chagua orodha ya Mkoa wa Songwe kutoka katika orodha zilizopo.
- Tafuta halmashauri yako husika ndani ya mkoa.
- Chagua shule uliyosoma.
- Pata orodha ya wanafunzi kutoka shule husika.
- Soma maelekezo ya kujiunga na Kidato cha Tano au chuo husika.
Kwa kuongezea, Uchaguzi wa Wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2025 umeandaliwa kwa mfumo kiwilaya na kimikoa. Kwa wilaya za Mkoa wa Songwe, orodha ya waliochaguliwa zinaweza inaweza kupatikana moja kwa moja kupitia kutumia linki za halmashauri z husika. Kupitia linki zifuatazo hapo chini utaweza kuona matokeo yao kwa haraka na usahihi zaidi.
- CHAGUA HALMASHAURI
ILEJE DC
MBOZI DC
MOMBA DC
SONGWE DC
TUNDUMA TC
2 Jinsi ya Kupata Maelekezo ya Kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi Mkoa wa Songwe
Baada ya kupata taarifa ya Form Five Selection Songwe, hatua zinazofuata ili kufanikisha safari yako ya elimu ya sekondari ya juu au chuo cha kati ni kupata maelekezo ya kujiunga kwa kufuata hatua hatua zifuatazo.
- Nenda kwenye tovuti ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz.
- Angalia kama umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano au chuo.
- Bofya kwenye linki ya jina la shule au chuo kushoto ili kupakua maelekezo ya kujiunga.
Fomu za maelekezo ya kujiunga zinapaswa kupakuliwa na kuchapishwa kama maelezo ya kujiunga na kujua mahitaji na tarehe za kuripoti shuleni au chuoni, pamoja na nyaraka zote muhimu unazotakiwa kwenda nazo. Mwanzo mzuri wa elimu ya Kidato cha Tano au chuo chako ni muhimu kwa mafanikio yako ya baadaye!
Kwa taarifa zaidi na msaada wa ziada, tafadhali rejea kwenye tovuti ya TAMISEMI au NACTVET kwa maelezo na huduma zaidi.