Table of Contents
Kila mwisho wa mwaka mara baada ya matokeo ya darasa la saba kutangazwa. NECTA kwa kushirikiana na TAMISEMI hufanya uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2025. Katika mchakato huu, wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba (PSLE) hupangiwa shule kulingana na alama zao na nafasi zilizopo katika shule za upili za serikali. Mchakato huu unasimamiwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na NECTA ili kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) anapangiwa kidato cha kwanza katika shule za seondari za serikali. Katika Makala hii tutachambua kwa kina jinsi kuangalia uchaguzi wa kidato cha kwanza, vigezo vinavyotumika na namna ya kupakua fomu za maelekezo ya kujiunga na kidato cha kwanza 2025.
Mchakato wa Uchaguzi wa kidato cha kwanza na Vigezo vinavyotumika kupanga shule wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2025
Uchaguzi wa Wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2025, umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE). Kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa Shule ya Sekondari ya Serikali.
Mwanafunzi mwenye Alama za juu anapata fursa ya kuchaguliwa katika shule za vipaji au za bweni. Wanafunzi wenye Ufaulu Mzuri zaidi Hupangiwa kwenye Shule za Sekondari za Bweni, Shule za Sekondari za Bweni Ufundi na Shule za Sekondari za Bweni Kawaida. Hivyo, Wanafunzi wenye alama nzuri wanajiongezea nafasi ya kchaguliwa katika shule nzuri zaidi Shule za Sekondari za Bweni na Shule za Sekondari za Bweni Ufundi. Utaratibuna vigezo vya kuwapangia wanafunzi katika shule hizo ni kama ifuatavyo.
- Shule za Sekondari za Bweni kwa Wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi; Nafasi katika shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi hugawanywa kwa kila Mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa wa Darasa la Saba waliosajiliwa katika Mkoa husika kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa. Nafasi zinazotolewa kwa Mkoa hugawanywa sawa kwa Halmashauri zote bila kujali idadi ya watahiniwa waliosajiliwa katika Halmashauri. Shule hizi zipo saba (7) ambazo ni Msalato, Mzumbe, Kilakala, Kibaha, Ilboru, Tabora Wasichana na Tabora Wavulana.
- Shule za Sekondari za Bweni Ufundi; Nafasi katika shule za Sekondari za Ufundi hugawanywa kwa kila Mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa wa Darasa la Saba waliosajiliwa kwa Mkoa husika kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa. Nafasi zinazotolewa kwa Mkoa hugawanywa sawa kwa kila Halmashauri bila kujali idadi ya watahiniwa waliosajiliwa katika Halmashauri.
- Shule za Sekondari za Bweni Kawaida; Nafasi katika Shule za Bweni za Kawaida za Kitaifa hugawanywa kwa kila Halmashauri kwa kufuata idadi ya watahiniwa wa darasa la Saba waliotoka katika mazingira magumu tu kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo kitaifa. Katika kundi hilo, Wanafunzi kutoka Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji hawasishwi isipokuwa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Orodha ya wanafunzi hupangwa kulingana na ufaulu wao kwa jinsi (order of merit) na waliofaulu Zaidi hupangwa shule za bweni kulingana na nafasi zilizopo kwenye Halmashauri husika.
1 Jinsi ya kuangalia Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2025
Utaratibu wa kuangalia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza kwa mwaka 2025 umerahisishwa kupitia mfumo maalum wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza kupitia Tovuti ya rasmi ya TAMISEMI. Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kuangalia orodha ya wanafunzi shule walizochaguliwa kidato cha kwanza 2025:
- Tembelea Tovuti ya TAMISEMI: Fungua kivinjari chako na andika www.tamisemi.go.tz. au https://selection.tamisemi.go.tz/
- Tafuta Sehemu ya ‘Announcements’ au ‘Matangazo’: Mara nyingi, TAMISEMI hutumia sehemu hii kutoa taarifa muhimu. Angalia kwa makini matangazo yanayohusiana na uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2025.
- Bofya kwenye liki ya “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025” au “Selection Form one 2025“: Utaelekezwa kwenye ukurasa maalum wa kuangalia orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa.
- Chagua Mkoa Wako: Mara baada ya kuingia kwenye ukurasa wa Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025, utakutana na orodha ya mikoa yote. Chagua mkoa ambao unataka kuona orodha ya wanafunzi waliochaguliwa.
- Chagua Halmashauri, Mara baada ya kuchagua mkoa, utaona Orodha ya Halmashauri za mkoa Husika, chaguo la Halmashauri husika ili kuona orodha ya shule katika Halmashauri husika.
- Chagua Shule Uliyosoma: Mara baada ya kuchagua Halmashauri, utapelekwa kwenye ukurasa wenye Orodha ya shule zote za Halmashauri Husika, chagua shule husika ambayo umefanyia Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 ili kuona orodha ya wanafunzi waliochaguliwa katika shule husika.
- Tafuta Jina lamwanafunzi au Mtahiniwa:Tafuta jina la mwanafunzi kwa kuiingiza jina la mwanafunzi kwenye kibox cha ku ‘search’ kwenye ukurasa huo
- Pakua Majina katika PDF kwa ajili ya matumizi ya baadaye: Unaweza kupakua pia Orodha ya majina katika mfumo wa faili la PDF. Kwa ajili ya matumizi ya baadaye Hakikisha una programu inayoweza kufungua faili za PDF kwenye kifaa chako. Pakua orodha na uanze kutafuta jina la mwanafunzi husika.
Kwa kufuata hatua hizi, utaweza kujua kwa urahisi iwapo mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kuanza maandalizi kwa ajili ya kuripoti katika shule aliyochaguliwa. Hakikisha unatembelea mara kwa mara tovuti ya TAMISEMI kwa matangazo mapya na Taarifa zaidi.
2 Orodha ya Majina ya waliochaguliwa kidato cha kwanza 2025 Kimkoa
Baada ya TAMISEMI kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025. Orodha Kamili imewekwa kwenye Tovuti ya TAMISMI ili wazazi na wanafunzi waweze kuangalia. Orodha hiyo imepangwa kimkoa, ili kurahisisha wazazi na wanafunzi kuona majina ya wanafunzi waliochaguliwa katika mikoa yao. Ili kupata orodha ya majina kimkoa tafadhali bofya linki ya mkoa Husika hapo chini:
3 Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 (form one joining instructions 2025)
Baada ya kutangazwa kwa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2025, hatua inayofuata ni kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 kwa shule husika. Maelekezo haya yanatoa taarifa muhimu kama vile taratibu za usajili, mahitaji ya shule, na tarehe za kuripoti shuleni. Kupakua maelekezo ya kujiunga na kidato cha kwanza 2025 fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea Tovuti ya NECTA: Kwa kawaida, maelekezo haya yatapatikana kwenye tovuti ya Baraza La Mtihani Tanzania (NECTA): https://onlinesys.necta.go.tz/
- Nenda kwenye Sehemu ya ‘News’; Mara nyingi, maelekezo na nyaraka zingine muhimu zinawekwa katika sehemu ya habari. Tafuta linki iliyoandikwa “Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025”.
- Tafuta jina la shule husika ili kupakua “MAELEKEZO YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA” Kwa shule Husika.
- Pakua Maelekezo Ya Kujiunga Kidato Cha Kwanza kwa kubofya linki ya shule husika: Mara baada ya kupata Jina la shule husika, bofya kwenye kiungo che ye jina la shule ili kuanza kupakua nyaraka hiyo kwenye kompyuta au simu yako.
- Soma Maelekezo Kwa Makini: Baada ya kupakua nyaraka, ifungue na kuisoma kwa makini. Maelekezo hayo yatakuwa na taarifa zote muhimu unazohitaji kujua kuhusu usajili, siku ya kuanza shule, vifaa vitakavyohitajika, na maelezo mengine ya msingi.
Kufuata hatua hizi kutakusaidia kupata maelekezo ya kujiunga na kidato cha kwanza, hivyo kuhakikisha kwamba taratibu zote zinafuatwa kwa usahihi na kwa wakati. Ni muhimu kuwa na taarifa sahihi ili kuepuka mkanganyiko wowote unaweza kujitokeza siku za usoni.
Shulewa lizohitimudarasalasabakwendaformone
Joining instructions ya ilboru sec naomba