Uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati kwa mwaka 2025 katika mkoa wa Dar es Salaam ni tukio muhimu kwa wanafunzi na wazazi. Ni wakati ambao wanafunzi waliohitimu Kidato cha Nne mwaka 2024 wanapata nafasi ya kuendeleza safari yao ya elimu. Mkoa wa Dar es Salaam, ulio miongoni mwa mikoa maarufu Tanzania, unajivunia maendeleo ya kibiashara na kijamii. Dar es Salaam ni kituo kikubwa cha kibiashara na mji wenye mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa.
Mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha Tano ulijumuisha wahitimu wa Kidato cha Nne kubadili machaguo ya Tahasusi za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo kupitia Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS). Mfumo huu umerahisisha uchaguzi kwa wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Serikali, huku ukitoa nafasi ya kufanya mabadiliko kwenye machaguo yao kabla ya kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, Mkoa wa Dar es Salaam
Kwa kawaida, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa pamoja na fomu za kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2025 inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTVET) www.nactvet.go.tz. Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) pia unapatikana kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Zifuatazo ni Hatua kwa hatua Jinsi ya kuangalia majina hayo:
- Tembelea Tovuti Rasmi: Fungua tovuti ya TAMISEMI ukitumia kivinjari chako.
- Bofya kwenye kiungo cha “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2025”.
- Fungua Linki ya Form Five First Selection 2025: Chagua kiunganishi kinachohusiana na chaguzi za mwaka 2025.
- Chagua Mkoa: Kutoka kwenye orodha ya mikoa, chagua “Dar es Salaam”.
- Chagua Halmashauri: Baada ya kuchagua mkoa, endelea kwa kuchagua halmashauri husika.
- Chagua Shule Uliyosoma: Teua shule ambapo ulisoma Kidato cha Nne.
- Pata Orodha ya Wanafunzi: Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa itajitokeza pamoja na maelekezo ya kujiunga.
Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 Dar es Salaam – Halmashauri zote
Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa mwaka 2025 unapangiliwa kiwilaya katika mkoa wa Dar es Salaam. Hivyo, ni wanafunzi wanaweza kuangalia moja kwa moja kupitia Halmashauri husika ili kupata matokeo sahihi na kwa urahisi zaidi. Hapa chini ni jedwali linaloonyesha wilaya zinazopatikana Dar es Salaam:
Kwa kubofya kiungo husika cha wilaya unayopendelea, utaweza kuona matokeo ya uchaguzi moja kwa moja.
- ILALA MC
- KIGAMBONI MC
- KINONDONI MC
- TEMEKE MC
- UBUNGO MC
Jinsi Ya Kupata Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 Dar es Salaam
Wanafunzi walioteuliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2025 katika Dar es Salaam wanaweza kupata maelekezo ya kujiunga kwa urahisi.
Baada ya kuFungua Tovuti ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz na kuapata Kufahama kama umechaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi.
Unatakiwa kuBofya linki ya Jina la Shule/Chuo ili kupakua maelekezo ya kujiunga.