Table of Contents
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya kati kwa mwaka 2025 katika mkoa wa Kagera ni tukio muhimu ambalo lilihusisha kutoa fursa ka wahitimu wa kidato cha nne 2024 kubadilisha machaguo yao ya tahasusi za kidato cha tano na kozi za vyuo vya ualimu, vyuo vya kati, na elimu ya ufundi kupitia mfumo wa Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS). Baada ya mchakato wa form five selection kukamilika majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya serikali yatatangazwa kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI na NACTE.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Kati, Katika mkoa wa Kagera
Kama ilivyo kawaida, matokeo ya uchaguzi wa kidato cha tano na vyuo vya kati katika mkoa wa Kagera yanaweza kupatikana kupitia tovuti rasmi za ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) (www.nactvet.go.tz) na kupitia Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz.
Kuangalia majina hayo, ingia kwenye tovuti ya Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Student Selection MIS) inayohusika na mchakato wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo vya kati (https://selform.tamisemi.go.tz/content/selection-and-allocation/). Fungua linki ya “form five First Selection, 2025”, kisha chagua Mkoa wa Kagera kutoka kwenye orodha ya mikoa. Utachagua halmashauri husika ndani ya mkoa, kisha shule uliyosoma, na mwishowe utaweza kupata orodha ya wanafunzi na maelekezo ya kujiunga.
1 Kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 kupitia linki za Halmashauri za Mkoa wa Kagera
Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka 2025 umepangiliwa kiwilaya.
- BIHARAMULO DC
- BUKOBA DC B
- UKOBA MC
- KARAGWE DC
- KYERWA DC
- MISSENYI DC
- MULEBA DC
- NGARA DC
2 Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Elimu Ya Ufundi 2025 mkoa wa Kagera
Baada ya kuthibitisha kwamba umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano au chuo cha elimu ya ufundi katika mkoa wa Kagera, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga. Tembelea tovuti ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz) ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hizi. Unachotakiwa kufanya ni kubofya kwenye jina la shule au chuo ili kupakua maelekezo hayo.
Kwa mfano, baada ya kuingia kwenye tovuti na kuchagua mkoa wa Kagera, tafuta shule au chuo ulichopangiwa. Ukishaona, utabonyeza jina hilo moja kwa moja kuweza kuona na kupakua fomu ya maelekezo ambayo itakusaidia katika kufahamu hatua zote za kujiunga na taasisi hiyo ya elimu.