Table of Contents
Mwaka 2025 umekuwa mwaka muhimu kwa wanafunzi wa darasa la saba 2024 nchini Tanzania, kwani ni wakati ambao matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza yanatangazwa. Katika mkoa wa Iringa, wazazi na wanafunzi wana hamu kubwa ya kujua shule ambazo wanafunzi wamepangiwa kuanza kidato cha kwanza. Uchaguzi huu ni matokeo ya juhudi na bidii ya wanafunzi katika mitihani yao ya mwisho ya elimu ya msingi. Mchakato huu unaratibiwa na TAMISEMI na unalenga kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata nafasi katika shule inayofaa kulingana na matokeo yao.
Jinsi ya kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 Mkoa wa Iringa
Kusubiri matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza kunaweza kuwa ni kipindi cha wasiwasi kwa wazazi na wanafunzi. Hata hivyo, mchakato wa kuangalia matokeo haya umefanywa kuwa rahisi na wa moja kwa moja. Hapa chini ni hatua za kufuata ili kuangalia matokeo ya Form One Selection 2025 kwa mkoa wa Iringa:
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
- Nenda kwenye kipengele cha ‘Matangazo’.
- Bofya linki ya “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025”
- Ukurasa Mpya utafunguka kisha chagua mkoa wa Iringa.
- Chagua Halmashauri
- Chagua Shule Uliyosoma
- Tafuta jina la mwanafunzi katika orodha iliyotolewa.
Jinsi ya kuangalia Majina ya waliochaguliwa kidato cha kwanza Kwa wilaya zote za mkoa wa Iringa
Mkoa wa Iringa una wilaya kadhaa, Wanafunzi na wazazi wanaweza pia kuangalia matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza kwa kuzingatia wilaya zao. Wilaya zinazopatikana katika mkoa wa Iringa ni pamoja na Iringa Mjini, Iringa Vijijini, Kilolo, na Mafinga. Kila wilaya ina orodha ya wanafunzi waliopangiwa shule mbalimbali ndani na nje ya wilaya hiyo.
1 Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 Iringa
Baada ya kujua shule ambayo mwanafunzi amechaguliwa kwa mwaka 2025, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga na shule hiyo. Hii ni muhimu kwani inatoa taarifa zote muhimu zinazohitajika kabla ya kuripoti shule, ikiwemo mahitaji ya shule na tarehe za kuripoti.
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.matokeo.necta.go.tz.
- Nenda kwenye sehemu ya “News”.
- Bofya linki ya “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025“.
- Tafuta jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi na kisha pakua maelekezo.