Mfumo wa TAMISEMI Selform ni mfumo wa kielektroniki ulioanzishwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa lengo la kusaidia wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Nne kubadilisha machaguo yao ya tahasusi na kozi za vyuo. Mfumo huu ni muhimu sana kwani unawapa wanafunzi nafasi ya kufanya mabadiliko kulingana na ufaulu wao. Hatua hii inakuja wakati serikali ikijiandaa kuchagua wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Tano na vyuo vya serikali mwaka 2025. Kupitia mfumo huu, serikali inatoa fursa kwa wahitimu kuboresha machaguo yao ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao kwenye mtihani wa Kidato cha Nne 2024
Jinsi Ya Kuingia na Kujisajili Kwenye Mfumo wa TAMISEMI Selform
Kuingia na kujisajili kwenye mfumo wa TAMISEMI Selform ni mchakato ambao umekuwa rahisi, wenye ufanisi, na unaolenga kusaidia wanafunzi kufanya mabadiliko ya machaguo yao ya masomo na kozi wanazotaka kusoma. Ikiwa wewe ni mhitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2024 na unataka kufanya mabadiliko kwenye machaguo yako, huu hapa ni mwongozo wa jinsi unavyoweza kufanya hivyo:

Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuingia
- Fungua Kivinjari Chako cha Mtandao: Ukiwa na upatikanaji wa mtandao, fungua kivinjari chako cha mtandao (mfano Google Chrome, Mozilla Firefox, n.k.).
- Andika Anuani ya Tovuti: Katika sehemu ya anuani ya kivinjari, andika: selform.tamisemi.go.tz na bonyeza kitufe cha kuenda (Enter) ili kufungua tovuti ya Selform.
- Jisajili kwenye Tovuti: Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuingia kwenye mfumo, bofya kwenye menu iliyoandikwa “For Candidates, click here to Register“. Hii itakufungulia fomu ya usajili ambapo utajaza taarifa zako za msingi.
- Jaza Taarifa Muhimu: Baada ya kufungua fomu ya usajili, utahitajika kujaza taarifa kama Namba ya Mtihani (Index Number) kwa mfano, S0101.0020.2018, jibu swali litakaloletwa, andika jina la ukoo na mwaka wa kuzaliwa. Hii itasaidia kuuthibitisha utambulisho wako.

- Chagua na Andika Nenosiri (Password): Mara baada ya kukamilisha usajili, mfumo utakutaka kuchagua na kuandika nenosiri utakaloendelea kutumia kila unapoingia kwenye akaunti yako. Hakikisha unachagua nenosiri ambalo ni ngumu kwa wengine kukisia lakini rahisi kwako kukumbuka.

- Ingia Tena kwa Kutumia Taarifa Mpya: Baada ya kubadili au kuthibitisha nenosiri lako, utahitaji kuingia tena kwenye mfumo kwa kutumia Namba yako ya Mtihani (Index Number) na nenosiri uliloandika.

Jinsi Ya Kuingia Na kubadili Tahasusi na Kozi za vyuo kwa Wahitimu wa Kidato cha Nne 2024
Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye mfumo wa TAMISEMI Selform, hatua inayofuata itakuwa ni kubadilisha machaguo yako ya masomo na vyuo. Hii ni hatua muhimu inayokuwezesha kuchagua kwa usahihi tahasusi na kozi unazotaka kusoma, kulingana na matokeo yako ya Kidato cha Nne. Ili kuhakikisha unafanya mabadiliko haya kwa ufanisi, fuata hatua hizi:
Taarifa Binafsi za Mwanafunzi
Mara baada ya kuingia kwenye akaunti yako, utakutana na dirisha la taarifa binafsi. Katika sehemu hii, utaweza kubadili taarifa zingine muhimu kama anwani ya nyumbani, namba ya simu, na barua pepe. Hakikisha unahifadhi taarifa zako mpya kwa kubonyeza kitufe cha ‘Save and Next’.

Machaguo ya Kawaida ya Mwanafunzi
Katika sehemu hii, utakuwa na uwezo wa kubadili machaguo yako ya awali ya shule na tahasusi. Chagua shule na tahasusi unazotamani kulingana na ufaulu wako. Ukifanya mabadiliko, kumbuka kubofya ‘SAVE & NEXT’ ili kuhifadhi na kuendelea.

Machaguo Mbadala
Sehemu hii ni maalum kwa ajili ya kubadilisha machaguo yako ya vyuo vya kisekta. Unaweza kuamua ni vyuo gani na kozi zipi ungependa kusoma, kama vile vyuo vya biashara, teknologia, na ufundi stadi. Ukimaliza kufanya mabadiliko, bofya ‘SAVE & NEXT’ ili kuhifadhi maendeleo yako.

Machaguo Maalum ya Shule za Kidato cha Tano
Hapa, unaweza kuchagua shule za Kidato cha Tano na tahasusi zake zilizo katika upeo wa ufaulu wako. Ni muhimu kukumbuka kuwa utaweza kuona tu machaguo ambayo yanalingana na ufaulu wako. Baada ya kutengeneza machaguo yako, bofya ‘SAVE & NEXT’ au ‘Save & Go Back’.

Elimu ya Ufundi
Katika sehemu hii, unaweza kubadilisha machaguo yako ya vyuo vya ufundi na tahasusi zake. Chagua programu ambazo zinaendana na ufaulu wako, hasa katika masomo ya PCM, ikiwa unataka kujiunga na kozi za ufundi kama uhandisi, teknolojia, n.k.

Elimu ya Afya
Kwa wale walio na matamanio ya kujiunga na vyuo vya afya, sehemu hii ni muhimu. Badilisha machaguo yako ili kuendana na vigezo na matokeo yako. Hakikisha unapanga ni kozi zipi za afya ambazo zinafaa zaidi kwako.

Elimu ya Diploma
Kama umepanga kuchukua masomo ya diploma, sehemu hii inakuwezesha kufanya mabadiliko ya tahasusi na vyuo vikuu vya diploma ambazo zinaendana na ufaulu wako.

Vyuo Vinginevyo
Sehemu ya mwisho hukuwezesha kufanya mabadiliko kwenye vyuo vingine ambavyo vinaweza kuwa na kozi za aina tofauti. Angalia machaguo mengine yanayoweza kufaa zaidi kwako.

Kwa kila hatua unayopitia, ni muhimu kuhakikisha kuwa unahifadhi mabadiliko yako kwa kubofya misimbo ya kuhifadhi. Mfumo huu umeundwa kurahisisha mchakato wa uchaguzi, hivyo hakikisha unatumia kila fursa ipasavyo kwa usahihi na umahiri. Wazazi na walezi wanaweza kusaidia katika kuchagua machaguo sahihi kwa ajili ya maendeleo bora ya mwanafunzi katika masomo yao ya juu.
Orodha ya Tahasusi za Kidato cha Tano
Kwa mwaka 2024, mfumo wa elimu wa Tanzania umeingiza mabadiliko makubwa katika tahasusi za Kidato cha Tano, lengo likiwa ni kupanua wigo wa uchaguzi kwa wanafunzi. Zifuatazo ni tahasusi mpya zilizowekwa ambazo zitawawezesha wanafunzi kupata maarifa katika maeneo mbalimbali ya masomo: Orodha hii inajumuisha:
TAHASUSI ZA SAYANSI YA JAMII
- History, Geography and Kiswahili (HGK)
- History, Geography and English Language (HGL)
- History, Geography and French (HGF)
- History, Kiswahili and English Language (HKL)
- History, Geography and Arabic (HGAr)
- History, Geography and Chinese (HGCh)
- History, Geography and Economics (HGE)
- History, Geography and Fasihi ya Kiswahili (HGFa)
- History, Geography and Literature in English (HGLi)
TAHASUSI ZA LUGHA
- Kiswahili, English Language and French (KLF)
- Kiswahili, English Language and Arabic (KLAr)
- Kiswahili, English Language and Chinese (KLCh)
- Kiswahili, Arabic and Chinese (KArCh)
- Kiswahili, Arabic and French (KArF)
- English Language, French and Arabic (LFAr)
- English Language, French and Chinese (LFCh)
- French, Arabic and Chinese (FArCh)
- History, English Language and French (HLF)
- History, English Language and Arabic (HLAr)
- History, English Language and Chinese (HLCh)
TAHASUSI ZA MASOMO YA BIASHARA
- Economics, Business Studies and Accountancy (EBuAc)
- Economics, Geography and Mathematics (EGM)
- Economics, Commerce and Accountancy (ECAc)
- Economics, Computer Science and Mathematics (ECsM)
- Business Studies, Accountancy and Computer Science (BuAcCs)
- Business Studies, Accountancy and Mathematics (BuAcM)
- Economics, Business Studies and Islamic Knowledge (EBuI)
TAHASUSI ZA SAYANSI
- Physics, Chemistry and Mathematics (PCM)
- Physics, Chemistry and Biology (PCB)
- Physics, Geography and Mathematics (PGM)
- Chemistry, Biology and Geography (CBG)
- Physics, Mathematics and Computer Science (PMCs)
- Chemistry, Biology and Agriculture (CBA)
- Chemistry, Biology and Food and Human Nutrition (CBN)
TAHASUSI ZA MICHEZO
- Biology, Food and Human Nutrition and Sports (BNS)
- English Language, Music and Sports (LMS)
- Kiswahili, Music and Sports (KMS)
- Fasihi ya Kiswahili, Music and Sports (FaMS)
- Literature in English, Music and Sports (LiMS)
- French, Music and Sports (FMS)
- Arabic, Music and Sports (ArMS)
TAHASUSI ZA SANAA
- Kiswahili, English Language and Theatre Arts (KLT)
- Kiswahili, French and Theatre Arts (KFT)
- Fasihi ya Kiswahili, English Language and Theatre Arts (FaLT)
- Kiswahili, Literature in English and Theatre Arts (KLiT)
- Kiswahili, English Language and Music (KLM)
- Kiswahili, French and Music (KFM)
- Fasihi ya Kiswahili, English Language and Music (FaLM)
- Kiswahili, Literature in English and Music (KLiM)
- Kiswahili, English Language and Fine Art (KLFi)
- Kiswahili, French and Fine Art (KFFi)
- Fasihi ya Kiswahili, English Language and Fine Art (FaLFi)
- Kiswahili, Literature in English and Fine Art (KLiFi)
- Kiswahili, Textile and Garment Construction and Fine Art (KTeFi)
- English Language, Textile and Garment Construction and Fine Art (LTeFi)
- Arabic, Textile and Garment Construction and Fine Art (ArTeFi)
- Chinese, Textile and Garment Construction and Fine Art (ChiTeFi)
TAHASUSI ZA ELIMU YA DINI
- Islamic Knowledge, History and Geography (IHG)
- Divinity, History and Geography (DHG)
- Islamic Knowledge, History and Arabic (IHAr)
- Divinity, History and English Language (DHL)
- Islamic Knowledge, History and English Language (IHL)
- Divinity, History and Kiswahili (DHK)
- Islamic Knowledge, History and Kiswahili (IHK)
- Divinity, Kiswahili and English Language (DKL)
kwa maelekezo zaidi pakua MUONGOZO WA MWANAFUNZI KATIKA MFUMO WA SELFORM NAMNA YA KUINGIA NA KUBADILISHA MACHAGUO pdf
Hitimisho
Mfumo wa TAMISEMI Selform unatoa nafasi kwa wanafunzi kubadili machaguo yao ili waweze kuchagua tahasusi na kozi zinazowakidhi mahitaji na uwezo wao. Ni muhimu kuchukua nafasi hii kwa umakini na kuzingatia ufaulu uliofikiwa ili kuhakikisha unajiandaa vyema kwa masomo ya Kidato cha Tano na kozi za vyuo ulivyovichagua. Mfumo huu una lengo la kuwawezesha watanzania vijana kupata elimu bora inayolingana na soko la ajira na mahitaji ya taifa. Usisahau ushauriane na wazazi wako au walezi katika kufanya maamuzi haya muhimu kwa maisha yako ya baadaye.