Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne. Katika makala hii, tutajadili utaratibu wa kutuma maombi ya ajira za polisi Tanzania, sifa zinazohitajika, na hatua za kufuata ili kuwa miongoni mwa waliofanikiwa kujipatia nafasi hizi muhimu.
Utaratibu wa Kutuma Maombi
Utaratibu wa kutuma maombi umewekwa ili kuwawezesha waombaji kuwasilisha maombi yao kwa ufanisi na kwa njia sahihi. Utaratibu wa kutuma maombi ni kama ifuatavyo:
- Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA. Barua hiyo iambatishwe kwenye maombi ikiwa kwenye mfumo wa ‘pdf’.
- Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) unaopatikana kwenye kiunganishi (link) cha tovuti ya Jeshi la Polisi (https://ajira.tpf.go.tz).
- Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta, barua pepe (email) au kwa mkono hayatapokelewa.
Kutuma maombi ya Online tafadhali tembelea linki; Jinsi ya Kutuma Maombi ya Ajira za Polisi Online
Muda wa mwisho wa Kuwasilisha Maombi:
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04/04/2025. Waombaji wanapaswa kufuata tarehe hii ili kuepusha kukosa nafasi ya kuzingatiwa.