Table of Contents
Mwaka 2025 unapoanza, wazazi na walezi katika mkoa wa Katavi wana hamu kubwa ya kujua ni wapi watoto wao waliofaulu mtihani wa darasa la saba watakapopangiwa kujiunga na kidato cha kwanza. Uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza ni hatua muhimu inayowezesha watoto kuanza safari yao ya elimu ya sekondari. Kwa mkoa wa Katavi, mchakato huu unaratibiwa na TAMISEMI, ambao hutoa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondari katika mkoa huo. Makala hii itakuelekeza jinsi ya kutazama matokeo ya uchaguzi huo kwa mwaka 2025.
Jinsi ya kuangalia Uchaguzi Wa Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza, 2025 Mkoa wa Katavi
Kuna njia kadhaa za kuangalia matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza katika mkoa wa Katavi:
Tovuti ya TAMISEMI
Njia rahisi na ya haraka ya kuangalia matokeo ni kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI (https://www.tamisemi.go.tz/). Mara matokeo yanapokuwa tayari, utapata kiungo kinachokuelekeza kwenye orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kwa mkoa wa Katavi.
- Tembelea tovuti rasmi ya TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).
- Nenda kwenye sehemu ya “Matangazo”.
- Bonyeza tangazo linalosema “UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025”, ukurasa mpya utafunguaka na kisha chagua mkoa wa Katavi.
- Chagua Halmashauri
- Chagua Shule Uliyosoma
- Tafuta jina la mwanafunzi katika orodha iliyotolewa.
Tovuti ya Wilaya:
Unaweza pia kutembelea ya wilaya husika. Orodha za wanafunzi waliochaguliwa hupakiwa kwenye tovuti hizi mara tu zinapokuwa tayari.
Shule za Msingi:
Shule nyingi za msingi pia hupokea orodha za matokeo ya uchaguzi na kuzibandika kwenye mbao za matangazo. Hii ni njia nyingine rahisi ya kupata matokeo.
1 Jinsi ya kuangalia Majina ya waliochaguliwa kidato cha kwanza Kwa wilaya zote za mkoa wa Katavi
Mkoa wa Katavi una wilaya mbalimbali, na uchaguzi wa wanafunzi huandaliwa kwa kuzingatia wilaya hizo. Ili kuhakikisha unapata matokeo sahihi, unaweza kuangalia uchaguzi wa kidato cha kwanza kwa wilaya husika kama ifuatavyo:
Kwa kila wilaya, utapata orodha ya shule na wanafunzi waliopangiwa katika shule hizo. Hii inasaidia sana ikiwa unataka kujua shule maalum alikopangiwa mwanao.
2 Jinsi ya kupakua Maelekezo Ya Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza 2025 Katavi – download Form One Joining Instructions for Katavi Region Schools
Baada ya kujua shule alikopangiwa mwanafunzi, hatua inayofuata ni kupakua maelekezo ya kujiunga na kidato cha kwanza. Haya maelekezo yanapatikana kupitia tovuti ya TAMISEMI, NECTA au unaweza kuyapata moja kwa moja kutoka kwenye tovuti za Halmashauri Husika. Maelekezo haya ni muhimu kwani yanatoa mwongozo wa vitu vinavyohitajika kabla ya kuanza masomo, kama vile ada, vifaa vya shule, na tarehe za kufika shuleni. Ili kupakua maelekezo haya, fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.matokeo.necta.go.tz.
- Nenda kwenye sehemu ya “News”.
- Bofya linki ya “MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2025“.
- Tafuta jina la shule aliyopangiwa mwanafunzi na kisha pakua maelekezo.
Kwa kuzingatia hatua hizi, wazazi na wanafunzi wa Katavi wataweza kujiandaa kikamilifu kwa safari mpya ya elimu ya sekondari. Tunawatakia kila la heri wote waliofanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2025!