Katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeendelea na mchakato wa uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mbalimbali nchini. Jimbo la Bunda, lililopo katika Mkoa wa Mara, nalo limejumuishwa katika orodha ya majimbo yaliyotangaza majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili wa kusimamia uchaguzi.
Tarehe na Mahali pa Kufanyika kwa Usaili
Usaili wa kusimamia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Jimbo la Bunda umepangwa kufanyika tarehe 17 Oktoba 2025, kuanzia saa 2:00 asubuhi. Eneo la usaili litakuwa katika Ofisi za Klasta – Nyamuswa. Waombaji wote walioteuliwa wanatakiwa kufika kwa wakati ili kuepuka usumbufu na kuhakikisha mchakato unafanyika kwa ufanisi.
Orodha ya Majina ya Waombaji Walioitwa Kwenye Usaili
Orodha kamili ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili wa kusimamia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa Jimbo la Bunda inapatikana kupitia linki zifuatazo
MAJINA YA USAILI UCHAGUZI JIMBO LA BUNDA_compressed.pdf
Kwa maelezo zaidi na orodha kamili ya majina, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda au ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Bunda