Kwa madhumuni ya uendeshaji wa uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kikisomwa pamoja na kanuni ya 11 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Nzega Vijijini na Bukene anawatangazia waombaji wafuatao kufika kwenye usaili Tarehe 15 Oktoba, 2025 siku ya Jumatano katika Vituo vya Usaili vinavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Wasailiwa wote wanaelekezwa kuzingatia muda wa kufika kwenye usaili bila kuchelewa na usaili utaanza saa 1:30 Asubuhi kwa Kila kituo cha Usaili.
