Table of Contents
Matokeo ya Darasa la Nne 2024 ni matokeo ya mtihani wa Upimaji Wa Kitaifa Wa Darasa La Nne (SFNA) kwa mwaka uliofanyika kwa muda wa siku mbili nchi nzima kuanzia tarehe 23/10/2024 hadi 24/10/2024. Mtihani huu unasimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na unalenga kupima uelewa na ustadi wa wanafunzi katika masomo ya msingi kama vile Hisabati, Uraia Na Maadili, Sayansi Na Teknolojia, Kiswahili, Kiingereza, na Maarifa ya Jamii.
Kutangazwa kwa Matokeo Darasa la Nne 2024 ni tukio muhimu katika mfumo wa elimu nchini Tanzania. Matokeo Matokeo ya Darasa la Nne yanatoa tathmini ya awali juu ya maendeleo ya wanafunzi katika hatua zao za mwanzo kielimu. Matokeo haya yanachukuliwa kwa umakini mkubwa kwani yanasaidia kujenga msingi imara kwa wanafunzi watakapokuwa wanajiandaa kwa elimu ya sekondari. NECTA hutangaza matokeo haya kupitia tovuti yake rasmi ya www.necta.go.tz. Katika Makala hii tumekuwekea mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuangalia matokeo hayo kupitia tovuti ya NECTA.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne Kupitia Tovuti ya NECTA
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ndio chombo pekee chenye jukumu la kusimamia na kutangaza matokeo ya mitihani mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na matokeo ya darasa la nne 2024. Ili kutazama matokeo ya darasa la nne kupitia tovuti ya NECTA, unahitaji kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA: Kwanza, fungua kivinjari chako cha mtandao na uingie katika tovuti rasmi ya NECTA kwa kutumia anwani ya URL: www.necta.go.tz.
- Nenda kwenye Sehemu ya Habari au “News”: Mara baada ya kufungua tovuti ya NECTA, utaona sehemu Habari au “News” ambayo inapatikana upande wa kusho katika ukurasa wa nyumbani wa tovuti. Tafuta na bonyeza Kwenye linki ya Habari mpya inayohusu “MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024”
- Chagua Mkoa na Halmashauri Husika: Katika ukurasa wa matokeo, utahitajika kuchagua Mkoa na Halmashauri unayotaka kutazama matokeo. Tafuta na chagua mkoa husika ili kupata matokeo ya wilaya zote za mkoa huo.
- Chagua Wilaya unayotaka kuangalia Matokeo ili kuona Orodha ya shule zote zilizopo katika Halmashauri husika.
- Tafuta jina la shule na fungua linki ya shule husika, Matokeo ya darasa la nne katika shule husika yatafunguka, Tafuta jina la mwanafunzi husika ili kupata matokeo yake.
1 Matokeo Darasa la Nne 2024/2025 Kimkoa (Mikoa Yote)
Kwa kawaida Matokeo ya darasa la nne hutangazwa na kupangiliwa kwa utaratibu wa kimikoa na Halmashauri zote. Hii husaidia wazazi na wadau kulinganisha na kutathmini ubora wa elimu katika mikoa mbalimbali. Takribani shule zoe msingi kutoka Mikoa yote nchini Tanzania zimeshiriki katika Mtihani Wa Upimaji Wa Kitaifa Wa Darasa La Nne (SFNA) 2024. Baadhi ya mikoa imekuwa ikifanya vizuri zaidi katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kutokana na uwekezaji mkubwa katika elimu, uwepo kwa walimu wakutosha na wenye ujuzi na kujituma, pamoja na ushirikiano mzuri kati ya wazazi na walimu.
Kila mwaka, NECTA hutangaza matokeo ya mitihani wa darasa la nne ya kila mkoa kupitia tovuti yake Rasmi. Wazazi na wanafunzi, wanaweza kuangalia matokeo haya kwa haraka kupitia linki zifuatazo hapo chini
Link to check: NECTA Standard Four Results 2024 – Link 01
2 Tafsiri ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Darasa la nne 2024/2025
NECTA hutumia alama na madaraja kutathmini kiwango cha ufaulu na uwezo wa mwanafunzi katika mitihani ya Darasa la nne. Ni muhimu kwa wazazi, walimu, na wanafunzi Kuelewa tafsiri ya alama na madaraja ili kujua ni wapi mwanafunzi amefanya vizuri na ni wapi anahitaji kuboresha. Zifuatazo ni tafsiri za Gredi na Alama za Matokeo ya darasa la nne
GREDI | ALAMA | MAELEZO |
A | 75-100 | Bora sana (Excellent): Hii ina maanisha kiwango bora zaidi ambacho mwanafunzi ameonyesha uelewa wa hali ya juu na uwezo wa kutumia maarifa kwa usahihi. |
B | 65-74 | Vizuri sana (Very Good): Hii inamaanisha uelewa mzuri ambapo mwanafunzi ameonyesha uwezo wa kutosha katika somo husika. |
C | 45-64 | Vizuri (Good): Kiwango hiki kinaonyesha uhusiano wa wastani wa uelewa na utekelezaji katika somo. Ni kiwango kinachokubalika lakini kuna nafasi ya kuboresha |
D | 30-44 | Inaridhisha (Satisfactory): Mwanafunzi ameonyesha kiwango cha kawaida cha uelewa katika somo husika. Mwanafunzi amefanikiwa kufikia kiwango cha chini kinavyohitajika katika ufaulu, lakini bado hajaonyesha umahiri au uelewa wa kina. |
F | 0-29 | Feli (Fail): Hii inaonyesha kuwa mwanafunzi amepata alama ya chini ya kiwango kinachohitajika na huenda akahitajika kurudia mtihani au kushiriki masomo ya ziada |
3 Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Matokeo ya Darasa la Nne
Yafuatayo Hapa chini ni baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Matokeo ya Darasa la Nne
Je, Matokeo ya Darasa la Nne yanatoka lini?
Matokeo ya darasa la nne kwa kawaida hutangazwa na NECTA miezi michache baada ya mitihani kukamilika. Kwa mwaka 2024/2025, matokeo yanatarajiwa kutongazwa mwanzoni mwa mwezi Januari, 2025. Ni muhimu kufuatilia taarifa kutoka NECTA ili kupata tarehe sahihi yakuachiwa kwa matokeo haya.
Je, kuna ada ya kuangalia matokeo mtandaoni?
Hapana, hakuna ada yoyote inayotozwa kwa kuangalia matokeo ya darasa la nne kupitia tovuti ya NECTA. Hata hivyo, unahitaji kuwa na kifaa kilichowezeshwa na Huduma ya intaneti.
Nini kinatokea ikiwa mwanafunzi hajafaulu?
Ikiwa mwanafunzi hajafaulu, ni muhimu kujadili na walimu ili kubaini maeneo ambayo mwanafunzi anahitaji msaada zaidi. Shule nyingi hutoa programu za ziada za masomo ili kusaidia wanafunzi wanaohitaji msaada wa ziada.
Kwa kumalizia, matokeo ya darasa la nne ni hatua muhimu katika safari ya elimu ya mwanafunzi. Kutazama na kuelewa matokeo haya husaidia katika kupanga mikakati ya kuboresha elimu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora zaidi. Kwa wazazi, walimu, na wanafunzi, ni muhimu kufuatilia matokeo haya kwa karibu na kuchukua hatua zinazofaa ili kuboresha mafanikio ya elimu.