zoteforum.com
No Result
View All Result
  • Login
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
PRICING
JIUNGE
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
No Result
View All Result
zoteforum.com
No Result
View All Result

Matokeo ya Darasa la Nne 2025 (NECTA Standard four results)

Matokeo ya Darasa la Nne 2024/2025

Zoteforum by Zoteforum
January 6, 2026
in NECTA Matokeo, SFNA results

Table of Contents

  • 1. Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne Kupitia Tovuti ya NECTA
  • 2. Matokeo Darasa la Nne 2025/2026 Kimkoa (Mikoa Yote)
  • 3. Tafsiri ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Darasa la nne 2025/2026
  • 4. Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Matokeo ya Darasa la Nne

Matokeo ya Darasa la Nne 2025 ni matokeo ya mtihani wa Upimaji Wa Kitaifa Wa Darasa La Nne (SFNA) kwa mwaka uliofanyika kwa muda wa siku mbili nchi nzima kuanzia tarehe 22/10/2025 hadi 23/10/2025. Mtihani huu unasimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na unalenga kupima uelewa na ustadi wa wanafunzi katika masomo ya msingi kama vile Hisabati, Uraia Na Maadili, Sayansi Na Teknolojia, Kiswahili, Kiingereza, na Maarifa ya Jamii.

Kutangazwa kwa Matokeo Darasa la Nne 2025 ni tukio muhimu katika mfumo wa elimu nchini Tanzania. Matokeo Matokeo ya Darasa la Nne yanatoa tathmini ya awali juu ya maendeleo ya wanafunzi katika hatua zao za mwanzo kielimu. Matokeo haya yanachukuliwa kwa umakini mkubwa kwani yanasaidia kujenga msingi imara kwa wanafunzi watakapokuwa wanajiandaa kwa elimu ya sekondari. NECTA hutangaza matokeo haya kupitia tovuti yake rasmi ya www.necta.go.tz. Katika Makala hii tumekuwekea mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuangalia matokeo hayo kupitia tovuti ya NECTA.

1 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne Kupitia Tovuti ya NECTA

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ndio chombo pekee chenye jukumu la kusimamia na kutangaza matokeo ya mitihani mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na matokeo ya darasa la nne 2025. Ili kutazama matokeo ya darasa la nne kupitia tovuti ya NECTA, unahitaji kufuata hatua zifuatazo:

  • Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA: Kwanza, fungua kivinjari chako cha mtandao na uingie katika tovuti rasmi ya NECTA kwa kutumia anwani ya URL: www.necta.go.tz.
  • Nenda kwenye Sehemu ya Habari au “News”: Mara baada ya kufungua tovuti ya NECTA, utaona sehemu Habari au “News” ambayo inapatikana upande wa kusho katika ukurasa wa nyumbani wa tovuti. Tafuta na bonyeza Kwenye linki ya Habari mpya inayohusu “MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2025”
  • Chagua Mkoa na Halmashauri Husika: Katika ukurasa wa matokeo, utahitajika kuchagua Mkoa na Halmashauri unayotaka kutazama matokeo. Tafuta na chagua mkoa husika ili kupata matokeo ya wilaya zote za mkoa huo.
  • Chagua Wilaya unayotaka kuangalia Matokeo ili kuona Orodha ya shule zote zilizopo katika Halmashauri husika.
  • Tafuta jina la shule na fungua linki ya shule husika, Matokeo ya darasa la nne katika shule husika yatafunguka, Tafuta jina la mwanafunzi husika ili kupata matokeo yake.

2 Matokeo Darasa la Nne 2025/2026 Kimkoa (Mikoa Yote)

Kwa kawaida Matokeo ya darasa la nne hutangazwa na kupangiliwa kwa utaratibu wa kimikoa na Halmashauri zote. Hii husaidia wazazi na wadau kulinganisha na kutathmini ubora wa elimu katika mikoa mbalimbali. Takribani shule zoe msingi kutoka Mikoa yote nchini Tanzania zimeshiriki katika Mtihani Wa Upimaji Wa Kitaifa Wa Darasa La Nne (SFNA) 2025. Baadhi ya mikoa imekuwa ikifanya vizuri zaidi katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kutokana na uwekezaji mkubwa katika elimu, uwepo kwa walimu wakutosha na wenye ujuzi na kujituma, pamoja na ushirikiano mzuri kati ya wazazi na walimu.

Kila mwaka, NECTA hutangaza matokeo ya mitihani wa darasa la nne ya kila mkoa kupitia tovuti yake Rasmi.  Wazazi na wanafunzi, wanaweza kuangalia matokeo haya kwa haraka kupitia linki zifuatazo hapo chini

ADVERTISEMENT

Link to check: NECTA Standard Four Results 2025 – Link 01

ARUSHADAR ES SALAAMDODOMA
GEITAIRINGAKAGERA
KATAVIKIGOMAKILIMANJARO
LINDIMANYARAMARA
MBEYAMOROGOROMTWARA
MWANZANJOMBEPWANI
RUKWARUVUMASHINYANGA
SIMIYUSINGIDASONGWE
TABORATANGA

3 Tafsiri ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Darasa la nne 2025/2026

NECTA hutumia alama na madaraja kutathmini kiwango cha ufaulu na uwezo wa mwanafunzi katika mitihani ya Darasa la nne. Ni muhimu kwa wazazi, walimu, na wanafunzi Kuelewa tafsiri ya alama na madaraja ili kujua ni wapi mwanafunzi amefanya vizuri na ni wapi anahitaji kuboresha. Zifuatazo ni tafsiri za Gredi na Alama za Matokeo ya darasa la nne

GREDIALAMAMAELEZO
A75-100Bora sana (Excellent): Hii ina maanisha kiwango bora zaidi ambacho mwanafunzi ameonyesha uelewa wa hali ya juu na uwezo wa kutumia maarifa kwa usahihi.
B65-74Vizuri sana (Very Good): Hii inamaanisha uelewa mzuri ambapo mwanafunzi ameonyesha uwezo wa kutosha katika somo husika.
C45-64Vizuri (Good): Kiwango hiki kinaonyesha uhusiano wa wastani wa uelewa na utekelezaji katika somo. Ni kiwango kinachokubalika lakini kuna nafasi ya kuboresha
D30-44Inaridhisha (Satisfactory): Mwanafunzi ameonyesha kiwango cha kawaida cha uelewa katika somo husika. Mwanafunzi amefanikiwa kufikia kiwango cha chini kinavyohitajika katika ufaulu, lakini bado hajaonyesha umahiri au uelewa wa kina.  
F0-29Feli (Fail): Hii inaonyesha kuwa mwanafunzi amepata alama ya chini ya kiwango kinachohitajika na huenda akahitajika kurudia mtihani au kushiriki masomo ya ziada

4 Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Matokeo ya Darasa la Nne

Yafuatayo Hapa chini ni baadhi ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Matokeo ya Darasa la Nne

Je, Matokeo ya Darasa la Nne yanatoka lini?

Matokeo ya darasa la nne kwa kawaida hutangazwa na NECTA miezi michache baada ya mitihani kukamilika. Kwa mwaka 2025/2026, matokeo yanatarajiwa kutongazwa mwanzoni mwa mwezi Januari, 2026. Ni muhimu kufuatilia taarifa kutoka NECTA ili kupata tarehe sahihi yakuachiwa kwa matokeo haya.

Je, kuna ada ya kuangalia matokeo mtandaoni?

Hapana, hakuna ada yoyote inayotozwa kwa kuangalia matokeo ya darasa la nne kupitia tovuti ya NECTA. Hata hivyo, unahitaji kuwa na kifaa kilichowezeshwa na Huduma ya intaneti.

Nini kinatokea ikiwa mwanafunzi hajafaulu?

Ikiwa mwanafunzi hajafaulu, ni muhimu kujadili na walimu ili kubaini maeneo ambayo mwanafunzi anahitaji msaada zaidi. Shule nyingi hutoa programu za ziada za masomo ili kusaidia wanafunzi wanaohitaji msaada wa ziada.

Kwa kumalizia, matokeo ya darasa la nne ni hatua muhimu katika safari ya elimu ya mwanafunzi. Kutazama na kuelewa matokeo haya husaidia katika kupanga mikakati ya kuboresha elimu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora zaidi. Kwa wazazi, walimu, na wanafunzi, ni muhimu kufuatilia matokeo haya kwa karibu na kuchukua hatua zinazofaa ili kuboresha mafanikio ya elimu.

Usikose Kusoma na Hizi Pia

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026 PDF: Pakua Hapa na Jinsi ya Kuangalia (CSEE Results)

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 (Form Four Results 2025)

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026: Jinsi ya Kuangalia CSEE results 2025

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Mbeya

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 Songwe

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Singida

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Simiyu

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Shinyanga

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 Ruvuma

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 Rukwa

Load More
SendShareShareTweet
Zoteforum

Zoteforum

Karibu Zoteforum.com, Tovuti yako pekee inayokupasha habari na Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani.

Makala Nyingine zaidi

Matokeo ya Kidato cha nne 2024

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 (Form Four Results 2025)

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026: Jinsi ya Kuangalia CSEE results 2025

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025/2026: Jinsi ya Kuangalia CSEE results 2025

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Mbeya

Matokeo ya Kidato cha nne 2025 Songwe

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Singida

Matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Simiyu

Load More

Weka maoni yako hapa au Komenti kuhusu makala hiiCancel reply

  • About
  • Cart
  • Checkout
  • Contact
  • Download Mziki na Nyimbo mpya
  • Habari za Burudani
  • Habari za Elimu
  • Habari za Soka
  • Home
  • Matokeo Ya Mitihani Tanzania – NECTA – MOCK – VYUO
  • My account
  • Nafasi za Kazi 2024
  • Offerings
  • Shop
  • Subscription
Call us: +1 234 JEG THEME

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.