Table of Contents
Matokeo ya darasa la nne ni kipimo muhimu cha maendeleo ya elimu katika ngazi ya msingi Katika mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya wanafunzi waliofanya mitihani ya darasa la nne 2024, Wazazi, walezi, na wanafunzi wanaweza kutazama matokeo haya kupitia tovuti rasmi ya NECTA.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya la nne Mkoa wa Kagera Kupitia Tovuti ya NECTA
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ina jukumu la kutangaza matokeo ya mitihani yote ya kitaifa yakiwemo matokeo ya darasa la nne. Ili kuangalia matokeo ya darasa la nne kwa mkoa wa Kagera, fuata hatua zifuatazo
- Fungua kivinjari chako cha intaneti (kama Chrome, Firefox, au Edge) kwenye kompyuta au simu yako ya mkononi.
- Andika anwani ya tovuti ya NECTA kwenye sehemu ya kuandika URL: www.necta.go.tz
- Baada ya kufungua tovuti ya NECTA, nenda kwenye kipengele cha “news” ambacho kwa kawaida hupatikana kwenye upande wa kulia wa tovuti.
- Utaona orodha ya Habari na machapisho mbalimbali, Katika orodha iliyopo, chagua ” MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024.”
- Utapewa fursa ya kuchagua mkoa ili kupata matokeo ya mkoa husika.
- Tafuta chagua mkoa wa “Kagera” ili kuona wilaya zote za mkoa huu.
- Chagua Wilaya unayotaka kuangalia Matokeo ili kuona Orodha ya shule zote zilizopo katika Halmashauri husika.
- Tafuta jina la shule na fungua linki ya shule hiyo kwa kubofya link ya shule, Matokeo ya darasa la nne katika shule husika yatafunguka, Tafuta jina la mwanafunzi husika ili kupata matokeo yake.
Baada ya Kufuata hatua hizi utaweza kupata matokeo ya darasa la nne kwa mkoa wa Kagera kwa usahihi na kwa wakati.
1 Matokeo ya Darasa la Nne Wilaya zote za Mkoa wa Kagera
Mkoa wa Kagera unaundwa na wilaya mbalimbali, ikiwemo Bukoba Mjini, Bukoba Vijijini, Muleba, Ngara, Karagwe, Biharamulo, na Kyerwa. Kila moja ya wilaya hizi ina shule nyingi ambazo wanafunzi wake hufanya mtihani wa darasa la nne kila mwaka. kupata matokeo ya Halmashauri husika , chagua linki ya Halmashauri hapo chini.