Table of Contents
1 Matokeo ya Darasa la Saba Mtwara 2024
Mkoa wa Mtwara ni moja ya mikoa yenye utajiri wa historia na utamaduni nchini Tanzania. Katika sekta ya elimu, mkoa huu unafanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanikiwa katika masomo yao, hasa wakati wa mitihani ya darasa la saba. Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2024 yanatarajiwa na wanafunzi, wazazi, na wadau wa elimu katika mkoa wa Mtwara. Makala hii inakusudia kukuongoza jinsi unavyoweza kuangalia matokeo ya darasa la saba kiurahisi kwa mwaka huu.
2 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya la saba Mkoa wa Mtwara Kupitia Tovuti ya NECTA
Ili kuangalia matokeo ya darasa la saba kwa wanafunzi wa mkoa wa Mtwara kupitia tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), fuata hatua hizi:
- Fungua kivinjari cha intaneti kwenye simu yako au kompyuta.
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa anuani ifuatayo: http://www.necta.go.tz.
- Mara baada ya tovuti kufunguka, tafuta sehemu iliyoandikwa “Matokeo” katika ukurasa wa mwanzo.
- Bonyeza kwenye “Matokeo ya Darasa la Saba” kutoka kwenye orodha.
- Ukurasa wa matokeo utafunguka, chagua mwaka wa mtihani ambao ni “2024”.
- Ukurasa wa matokeo kimikoa utafunguka, chagua mkoa ambao ni “Mtwara”.
- Ukurasa wa matokeo kiwilaya za mikoa wa mtwara utafunguka, chagua wilaya ambao husika.
- Ukurasa wenye orodha ya shule katika Halmashauri utafunguka, bonyeza linki ya shule husika.
- Tafuta jina la mwanafunzi husika kupata matokeo.
- Matokeo yatakujia moja kwa moja kwenye skrini yako, ambapo unaweza kuyanakili au kuyachapisha kwa matumizi ya baadaye.
3 Matokeo ya Darasa la Saba Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara
Wilaya zote katika mkoa wa Mtwara, zikiwemo Mtwara Vijijini, Mtwara Mjini, Masasi, Nanyumbu, na Newala, ni sehemu muhimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na matokeo mazuri. Kila wilaya imekuwa ikijitahidi kwa kuimarisha miundombinu ya elimu na kuongeza ufanisi wa walimu ili kuboresha matokeo ya mitihani. Wanafunzi wanashauriwa kuwa na subira wakati matokeo yanapotangazwa na kujiandaa kwa ajili ya hatua inayofuata katika elimu yao ya sekondari.
PSLE-2024 EXAMINATION RESULTS, MKOA WA MTWARA
Kwa hiyo, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuendelea kuwatia moyo na kuwasaidia wanafunzi katika maandalizi ya safari ijayo ya elimu ya sekondari. Pia, wanashauriwa kufuatilia maelekezo na kutambua shule ambazo watoto wao wamepangiwa kujiunga na kidato cha kwanza 2025 na kuhakikisha wanaripoti shuleni kwa wakati. Matokeo haya ni mwanzo mpya kwa wanafunzi wa mkoa wa Mtwara na ni matarajio yetu kuwa wataendelea kufanya vizuri zaidi katika viwango vya juu vya elimu.
shabani