Matokeo Kidato cha Nne 2024, yanatarajiwa kutangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) mwezi Januri, 2025. Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha nne 2024/2025 ni moja ya matukio yanayovuta hisia na matarajio makubwa kwa wazazi, walimu na wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2024.
Kwa ujumla Mtihani wa kidato cha nne unapima uelewa na ujuzi wa wanafunzi ambao wameupata katika kipindi cha miaka minne ya elimu ya sekondari. Kwa mwaka 2024, mtihani huu ulifanyika kote nchini, ukihusisha masomo mbalimbali kama vile Hisabati, Kiswahili, Kiingereza, Biologia, Kemia, Fizikia na mengineyo. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ndilo linalosimamia utungaji, usimamizi, na utoaji wa matokeo ya mtihani huu wa kidato cha nne. Jumla ya wanafunzi 557,731 kutoka katika shule za sekondari 5585 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 961 walifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2024. Aidha, katika watahaniwa wa shule 557,731 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wavulana ni 250,562 sawa na asilimia 47.34 na wasichana ni 278,759 sawa na asilimia 52.66. Matokeo ya kidato cha nne huamua muelekeo wa baadaye wa elimu na fursa za kazi kwa wanafunzi.
Matokeo ya Form four huleta furaha kwa watahiniwa waliofanikiwa na kufikia matarajio yao ya ufaulu, lakini pia ni kipindi cha kutafakari kwa wale ambao hawakupata alama walizotarajia. Ni muhimu kuelewa kwamba, ingawa matokeo haya ni sehemu kuu ya safari ya kielimu, bado kuna fursa nyingi za kujifunza na kuboresha katika maeneo mbalimbali. Kwa mwaka 2024, Watanzania wanatarajia kuona maendeleo na mabadiliko chanya katika matokeo haya, yakiashiria ubora wa elimu na kujituma kwa wanafunzi na walimu nchini Tanzania.
Kupitia Makala hii ili utapata ufahamu zaidi kuhusu Jinsi ya Kuangalia Matokeo Kidato cha nne 2024 Kupitia Tovuti ya NECTA Pamoja na Tafsiri ya Alama na Madaraja yanayotumika Katika Matokeo ya Kidato cha nne (NECTA Form Four Results 2024)
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha nne Kupitia Tovuti ya NECTA
Teknolojia imeleta mapinduzi makubwa katika jinsi tunavyoweza kupata Habari mbalimbali, na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) linahakikisha kuwa matokeo ya mitihani yanapatikana kwa urahisi kupitia mtandao. Kuangalia matokeo ya CSEE kwa urahisi kupitia tovuti ya NECTA, tafadhali fuata Hatua zifuatazo.
- Tembelea Tovuti Rasmi ya NECTA: Hatua ya kwanza ni kutembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa kuingia kwenye kivinjari (browser) chako na kuandika anwani ya tovuti: www.necta.go.tz. Tovuti hii ni chanzo cha uhakika na salama cha kupata taarifa za matokeo ya mitihani yote inayoendeshwa na NECTA.
- Tafuta Sehemu ya Matokeo: Mara baada ya kufika kwenye ukurasa wa mwanzo wa tovuti, nenda kwenye menyu menyu kuu na Tafuta au bonyeza kwenye kiungo kinachoandikwa “Results” au “Matokeo”. Kiungo hiki kitakuonyesha orodha ya Mtaokeo ya mitihani yote ya NECTA.
- Chagua Aina ya Mtihani: Katika menyu ya matokeo, utaona orodha ya aina za mitihani. Chagua “CSEE” (Certificate of Secondary Education Examination) results ili kupata matokeo kidato cha nne,
- Chagua linki ya Matokeo ya Mwaka husika: Katika ukurasa wa matokeo ya kidato cha nne , utaona orodha ya matokeo ya form four na miaka ambayo matokeo yametolewa. Bonyeza linki ya matokeo ya CSEE kwa mwaka husika, ambao ni 2024.
- Tafuta Shule uliyosoma: Baada ya ukurasa wa Matokeo ya kidato cha nne 2024 kufunguka, utahitajika kutafuta jina la shule ili kuona matokeo. Mara tu baada ya matokeo ya shule kufunguka Utaweza kuona matokeo yako kwa kutafuta namba ya mtihani au “Form four Index Number” ambayo uliitumia wakati wa kufanya mtihani.
- Angalia na Pakua Matokeo: Matokeo ya mwanafunzi yataonekana kwenye skrini. Unaweza kuyachapisha au kuhifadhi kama faili kwenye kompyuta au simu yako kwa matumizi ya baadaye.
Ni muhimu kuwa na subira na kutambua kwamba wakati wa kutangazwa matokeo ya form four, tovuti ya NECTA inaweza kuwa na Watembeleaji wengi na kusababisha matokeo kushindwa kuonekana kwa wakati hivyo unashauriwa kujaribu kutembelea tovuti hiyo mara kwa mara endapo kutatokea matatizo ya upatikanaji.
Jinsi ya kutazama Matokeo ya form four 2024 kwa Mikoa Yote Tanzania
Matokeo ya kidato cha nne yana umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na wazazi nchini. Kwa mwaka 2024, NECTA imeboresha njia za utoaji wa matokeo ili kuhakikisha yanapatikana kwa urahisi na uharaka . Kutazama matokeo ya form four katika mkoa wako, tafadhali chagua linki ya mkoa husika na Tafuta shule uliyomalizia kidato cha nne 2024.
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |
Tafsiri ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Kidato cha nne 2024
Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa na NECTA, Jambo linalufuata ni wanafunzi, wazazi, na walimu kuelewa tafsiri ya alama na madaraja yaliyotumika katika matokeo hayo. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lina mfumo maalum wa kupanga alama na madaraja ambao husaida kutoa mwelekeo na tathmini ya kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Kwa mwaka 2024, Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne nchini Tanzania yamewasilishwa kwa mfumo wa alama, division, pointi na madaraja, ambao unasaidia kutoa tathmini ya ufaulu wa wanafunzi katika masomo yao.
Zifuatazo ni tafsiri za alama na madaraja katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2024.
GREDI | ALAMA | DARAJA | POINTI | MAELEZO |
A | 75-100 | I | 1-7 | Bora sana (Excellent): |
B | 65-74 | II | 18-21 | Vizuri sana (Very Good) |
C | 45-64 | III | 22-25 | Vizuri (Good) |
D | 30-44 | IV | 26-33 | Inaridhisha (Satisfactory) |
F | 0-29 | 0 (Zero) | 34-35 | Feli (Fail) |
Tafsiri sahihi ya alama na madaraja ni muhimu kwa wanafunzi na wazazi kwani husaidia kuelewa kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi na hatimaye kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wa elimu. Kwa mfano, ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu humuwezesha mwanafunzi kujiunga na masomo ya juu katika shule za sekondari za kidato cha tano na sita, pamoja na vyuo vya kati. Kwa upande mwingine, daraja la nne linamuwezesha mwanafunzi kujiunga na mafunzo ya ufundi na baadhi ya vyuo vya Diploma na cheti.
Kwa hivyo, kuelewa mfumo huu wa alama na madaraja husaidia wanafunzi na walezi kujipanga vizuri na kuchukua hatua zinazohitajika kwa ajili ya mipango ya baadaye ya kitaaluma. Pia, huwapa walimu mwongozo katika kutathmini na kuboresha mbinu zao za ufundishaji ili kuimarisha ufahamu wa wanafunzi na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa miaka ijayo.