Leo tarehe 23 Januari 2025, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Limetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2024. Dkt. Said A. Mohamed, Katibu Mtendaji wa NECTA, ametangaza matokeo hayo kupitia mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika katika Ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania iliyopo Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.

Habari njema kwa wanafunzi, wazazi, na walezi wote ambao wamekuwa wakisubiri kwa hamu matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hatimaye limetangaza matokeo haya leo, yakionesha jinsi gani wanafunzi walivyojitahidi katika mitihani yao. Matokeo haya ndio kigezo cha wanafunzi kujiunga na vyuo vya elimu ya juu, vyuo vya ufundi, au hata kuingia katika soko la ajira.
Linki za Kuangalia Matokeo
Baraza la Mitihani la Taifa limewezesha upatikanaji wa matokeo kwa njia rahisi na ya haraka kupitia mtandao. Unaweza kuyapata matokeo katika tovuti rasmi ya NECTA ambayo ni NECTA. Pia, matokeo yanaweza kuangaliwa kupitia SMS kwa kutuma namba ya usajili ya mwanafunzi kwenda namba iliyotolewa na Baraza.
Matokeo ya kidato cha nne 2024 yatapatikana kupitia linki zifutazo
- Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha nne 2024
- MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024 -LINKI YA NECTA
Matokeo ya kidato cha nne kwa Mikoa Yote Tanzania