Table of Contents
Matokeo ya Kidato cha Pili 2024 , haya ni matokeo rasmi ya Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa Wa Kidato Cha Pili (FTNA) 2024 ambayo hutolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kila mwaka miezi miwili baada ya wanafunzi wa kidato cha pili kufanya mitihani huo. Mitihani hii ni ya lazima katika mfumo wa elimu ya sekondari nchini na inatoa tathmini muhimu ya maendeleo ya elimu ya wanafunzi baada ya miaka miwili ya masomo katika ngazi ya sekondari.
Matokeo ya kidato cha pili 2024 yanatarajiwa kutoa tathmini ya uelewa wa wanafunzi katika masomo waliyofundishwa, na kutoa fursa kwa walimu na wazazi kuelewa maeneo ambayo wanafunzi wanahitaji msaada zaidi.
Matokeo ya kidato cha pili ya Mwaka 2024 yanasubiriwa kwa hamu kubwa sana kwa sababu yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa elimu kuangalia mabadiliko na maboresho yaliyofanywa katika mitaala na mbinu za ufundishaji. Kwa ujumla, Matokeo ya kidato cha pili yatatoa mwangaza juu ya mafanikio ya juhudi mbalimbali ambazo zimeendelea kufanywa na serikali katika Nyanja ya elimu nchini kiwa ni Pamoja na matumizi ya teknolojia katika madarasa hadi mbinu za kufundisha ambazo zinalenga kukuza ujuzi wa kufikiri kwa kina na kutatua matatizo yanayoizunguka jamii.
Kwa wazazi, hii ni fursa ya kupima maendeleo ya watoto wao na kubaini maeneo yanayohitaji msaada zaidi nyumbani. Vivyo hivyo, kwa walimu, matokeo haya yanaweza kutoa maoni muhimu katika kuboresha mbinu za kufundisha na kuimarisha maeneo yenye changamoto katika ufundishaji. Katika Makala hii utaweza kufahamu Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha pili Kupitia Tovuti ya NECTA na kuelewa Tafsiri ya Alama na Madaraja ambayo NECTA huyatumika Katika upangaji wa Matokeo ya mtihani wa Kidato cha pili
1 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha pili 2024 Mtandaoni
Katika ulimwengu wa maendeleo ya kidijitali, teknolojia imerahisisha upatikanaji wa taarifa za matokeo ya mitihani mbalimbali nchini. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeboresha utaratibu wa kutangaza matokeo kwa kuwezesha wanafunzi na wadau wengine wa elimu kuyaangalia kupitia tovuti yao rasmi. Ufuatao ni muongozo wa hatua kwa hatua jinsi ya kuangalia matokeo ya kidato cha pili 2024 kupitia tovuti ya NECTA.
Hatua ya 1: Fungua Tovuti ya NECTA
Kwanza, hakikisha kompyuta yako, simu au kifaa chochote cha kielektroniki unachotumia kimeunganishwa na mtandao wa intaneti. Kisha, fungua kivinjari chako cha intaneti na andika anwani ya tovuti ya NECTA, ambayo ni www.necta.go.tz, Utapelekwa kwenye ukurasa wa nyumbani wa tovuti ya NECTA
Hatua ya 2: Nenda kwenye Kipengele cha Habari au Matangazo
Mara baada ya kufungua tovuti, elekea kwenye sehemu ya ‘Habari au Matangazo’ ambayo mara nyingi hupatikana kwenye ukurasa wa mbele upande wa kulia wa tovuti ya NECTA. NECTA hutoa matangazo yote muhimu, ikiwemo matokeo ya mitihani katika kipengele hiki. Hapa, utapata kiungo au tangazo linalosema ” Matokeo Ya Upimaji Wa Kitaifa Wa Kidato Cha Pili (FTNA Results) 2024” au “Matokeo Ya Form Two 2024 “ Bonyeza kiungo hicho ili kuelekea kwenye ukurasa wa matokeo.
Hatua ya 3: Chagua Shule
Baada ya kufungua ukurasa wa matokeo ya Kidato cha Pili, orodha ya shule zote itaonekana. Chagua jina la shule yako au jina la shule unayohitaji kuona matokeo yake. Baada ya kufanya uchaguzi, matokeo ya wanafunzi wote kutoka shule hiyo yataonekana. Tafuta jina lako au namba yako ya mtihani kuangalia matokeo yako. Hakikisha unahifadhi nakala ya matokeo hayo kwa matumizi ya baadaye.
Kwa kufuata hatua hizi kwa umakini, utaweza kuona matokeo ya kidato cha pili kwa urahisi na bila usumbufu. Ni muhimu kuzingatia kwamba utumiaji wa tovuti rasmi ya NECTA ni njia salama na ya kuaminika ya kupata matokeo, hivyo epuka kutegemea tovuti zisizo rasmi au ambazo hazina uaminifu.
2 Matokeo ya Kiadato cha pili (form two 2024) kwa Mikoa Yote Tanzania
Kila mkoa una orodha ya shule zake. Unaweza kutazama matokeo ya kidato cha pili kwa utaratibu wa mikoa. NECTA inatoa linki maalum inayowezesha kuangalia matokeo ya form two moja kwa moja katika Mkoa Husika.
Utaratibu huu wa kutazama matokeo unarahisisha mchakato kwa wanafunzi, wazazi, na waalimu ambao wanahitaji kupata matokeo haraka na kwa usahihi. Kwa kutumia linki zifuatazo, anaweza kuona matokeo kwa uhakika na kuwa urahisi zaidi. Tutumia Linki rasmi kutoka NECTAili kuangalia matokeo Kidato cha pili.
FORM TWO NATIONAL ASSESSMENT (FTNA) 2024 RESULTS ENQUIRIES
Unaweza pia kutumia linki hii hapa: NECTA Form Two Results 2024 link 02
3 Tafsiri ya Alama na Madaraja Katika Matokeo ya Kidato cha pili 2024
NECTA imeweka mfumo maalum wa alama na madaraja ambao hutumika kupima kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi katika kila somo. Matokeo ya mitihani ya kidato cha pili nchini Tanzania yanawasilishwa kwa mfumo wa alama, division, pointi na madaraja, ambao unasaidia kutoa tathmini ya ufaulu wa wanafunzi katika masomo yao. Mfumo huu wa upangaji wa alama ni sehemu muhimu ya kuelewa jinsi mwanafunzi alivyofanya na ni miongozo ipi inayoweza kusaidia katika kuboresha zaidi mafanikio yao ya kitaaluma.
Zifuatazo ni tafsiri za alama na madaraja katika matokeo ya kidato cha pili ya mwaka 2024.
GREDI | ALAMA | DARAJA | POINTI | MAELEZO |
A | 75-100 | I | 1-7 | Bora sana (Excellent): |
B | 65-74 | II | 18-21 | Vizuri sana (Very Good) |
C | 45-64 | III | 22-25 | Vizuri (Good) |
D | 30-44 | IV | 26-33 | Inaridhisha (Satisfactory) |
F | 0-29 | 0 (Zero) | 34-35 | Feli (Fail) |