Mtihani wa kidato cha pili hutumika kupima uwezo wa wanafunzi katika masomo yaliyosomwa kwa miaka miwili ya mwanzo wa elimu ya sekondari na pia ni njia mojawapo ya kuwachuja ili kuwaruhusu kuendelea na masomo yao katika kidato cha tatu. Matokeo haya yana umuhimu mkubwa kwa mkoa wa Iringa kwani yanatumika kama kipimo cha ubora wa elimu inayotolewa na shule mbali mbali za sekondari katika mkoa huu. Matokeo ya kidato cha pili ni kigezo muhimu kinachotumiwa na wazazi na walezi kuchukua maamuzi juu ya mustakabali wa kielimu wa watoto wao. Zaidi ya hayo, yanaweza kusaidia kutambua nafasi ya mkoa wa Iringa kitaifa katika suala la elimu.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya form two kwa Wilaya zote za Mkoa wa Iringa
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeendelea kurahisisha mfumo wa kupata matokeo ya Kidato cha Pili kwa kutumia mtandao. Kwa wanafunzi na wazazi wa mkoa wa Iringa, matokeo haya yanaweza kupatikana kiurahisi kupitia tovuti rasmi ya NECTA. Kwa mkoa wa Iringa, wanafunzi na wazazi kufuatilia matokeo ya wilaya zao kupitia linki maalum zinazotolewa na NECTA. Ili kuangalia matokeo bofya linki ya wilaya husika, na chagua shule yako ili kuona orodha ya shule zilizopo kwenye wilaya hiyo:
Aidha namna nyingine ya kuangalia matokeo ya kidato cha pili ni kutembelea moja kwa moja tovuti ya NECTA kupitia anwani ifuatayo: www.necta.go.tz. Mara baada ya kufungua tovuti hiyo, utatafuta sehemu iliyoandikwa ‘Results’, kisha chagua kipengele cha ‘Form Two Results’. Katika orodha ya shule, tafuta na uchague shule yako. Ambapo unaweza kubofya linki husika na kuona matokeo yako.