Matokeo ya Kidato cha Pili kwa Mkoa wa Manyara ni kipimo muhimu cha ufanisi wa elimu kwa wanafunzi wanaomaliza ngazi ya pili ya sekondari. Hii ni hatua muhimu ambayo huwawezesha wanafunzi kuendelea na Kidato cha Tatu katika michepuo ya masomo kulingana na matokeo yao.
Mtihani huu, unasimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), huwapa wanafunzi fursa ya kuonyesha uwezo wao katika masomo mbalimbali kama Mathematics, Chemistry, Physics, Biology, Civics, English, Geography, History, Kiswahili. Matokeo Matokeo ya Kidato cha Pili yana umuhimu mkubwa kwasababu yanaakisi ubora wa elimu inayotolewa katika mkoa.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya form two kwa Wilaya zote za Mkoa wa Manyara
NECTA hutoa matokeo ya Kidato cha Pili kupitia tovuti yao rasmi. Wanafunzi, wazazi, na walezi wanaweza kuyapata matokeo haya kwa urahisi kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz.
- Katika menyu ya tovuti, bonyeza ‘Results’ kisha chagua ‘FTNA’ kutoka kwenye orodha ya menyu.
- Chagua ‘matokeo ya 2024’ kama mwaka wa matokeo unayotaka kuyaona.
- Baada ya ukurasa wa matokeo kufunguka utaona orodha ya shule, chagua shule husika kuona matokeo yake.
Kwa kila wilaya, NECTA inatoa kiungo cha moja kwa moja ambacho kinakuwezesha kuona matokeo kwa shule zote zilizopo katika wilaya hiyo. Ili kuona matokeo kwa wilaya husika tafadhali tumia linki ya Wilaya Husika