Table of Contents
Mkoa wa Shinyanga ni moja ya mikoa ya Tanzania ambapo wanafunzi hutahiniwa kila mwaka kwa ajili ya mtihani wa Kidato cha Pili. Mtihani wa kidato cha pili ni mtihani wa kitaifa unaoandaliwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na hufanyika mwishoni mwa mwaka wa pili wa masomo ya sekondari. Mtihani huu unatoa taswira ya maendeleo ya elimu ya wanafunzi kabla ya kuingia kidato cha tatu, Pia, Mtihani huu huwaandaa wanafunzi kwa masomo ya kidsto cha tatu na cha nne na pia huamua ikiwa wanafunzi wataendelea na kidato cha tatu. Matokeo ya mtihani huu yanasaidia pia katika kupima ubora wa elimu inayotolewa katika shule za sekondari za mkoa na kutoa mwongozo kwa walimu na wazazi kuhusu maeneo ya kuboresha.
1 Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya form two kwa Wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linatoa matokeo ya Kidato cha Pili kwa njia ya mtandao ambapo wanafunzi, walimu, na wazazi wanaweza kuyapata kwa urahisi. Kwa mkoa wa Shinyanga, matokeo haya yanaweza kuangaliwa moja kwa moja kupitia tovuti ya NECTA. Mara baada ya matokeo kutangazwa, unaweza kutembelea tovuti ya NECTA kwa kuandika www.necta.go.tz. Katika tovuti hiyo, kutakuwa na sehemu maalum ya ‘Matokeo’ ambapo utachagua ‘Matokeo ya Kidato cha Pili 2024’. Kisha, chagua shule husika.
Kwa urahisi zaidi, NECTA imetoa linki ya moja kwa moja ili kuwasaidia watu kupata matokeo kwa haraka ambapo linki zifuatazo zinaweza kutumika kuangalia matokeo.
Matokeo ya Kidato cha Pili ni muhimu sana kwa wanafunzi wa mkoa wa Shinyanga kwani yanaamua muelekeo wa masomo yao ya sekondari. Ni vyema kwa wanafunzi, wazazi na walimu kutumia matokeo haya kama chombo cha kujitathmini na kujua ni wapi pa kuboresha ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora zaidi. NECTA imehakikisha kuwa upatikanaji wa matokeo ni rahisi na haraka kupitia tovuti yao, hii inawezesha kila mdau katika sekta ya elimu kufuatilia matokeo hayo bila usumbufu.