zoteforum.com
No Result
View All Result
  • Login
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
PRICING
JIUNGE
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
No Result
View All Result
zoteforum.com
No Result
View All Result

NACTVET yafungua Dirisha La Udahili Wa kozi za Astashahada Na Stashahada Kwa Mwaka Wa Masomo 2025/2026

Zoteforum by Zoteforum
May 29, 2025
in NACTE

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na NACTVET umefunguliwa rasmi leo tarehe 28 Mei, 2025.

Maombi ya udahili kwa kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi, na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika vyuo vilivyoko Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 11 Julai, 2025.

Aidha, maombi ya kozi za Afya na Sayansi Shirikishi – Tanzania Bara, yatafanyika kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System-CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 11 Julai, 2025.

Baraza pia linautaarifu umma kuwa kozi zinazoombwa na vyuo vinavyotoa kozi hizo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026 (Admission Guidebook for Academic Year 2025/2026). Mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz).

Baraza linasisitiza kila mwombaji kuhusika mwenyewe katika zoezi zima la kuomba kudahiliwa, kuandika taarifa zake kwa usahihi na umakini, na kutunza kumbukumbu atakazopatiwa na Baraza kupitia namba yake ya simu, bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepuka usumbufu katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi/vyuo mbalimbali.

Mambo ya Kuzingatia kwa Wanaoomba Kupitia Mfumo wa Udhaili wa Pamoja (Central Admission System – CAS):

  1. Muombaji anaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja. Kuchaguliwa katika chuo alichoomba kutategemea ushindani utakaokuwepo katika chuo hicho.
  2. Muombaji akishachaguliwa, atapokea ujumbe kutoka NACTVET kupitia namba ya simu yake aliyoweka kwenye mfumo wakati wa kufanya maombi. Ujumbe huo utamjulisha kuwa amechaguliwa kujiunga na chuo fulani (jina la chuo), na utakuwa na msimbo (code) ambao atatakiwa kuutunza na kuuwasilisha kwa chuo alichochaguliwa siku atakapokwenda katika chuo hicho kwa ajili ya kuanza masomo.
  3. Baada ya kuwasilisha msimbo huo chuoni, atasajiliwa na chuo, kisha atapokea ujumbe kutoka NACTVET ukimueleza kuwa amesajiliwa.
  • Baada ya kusajiliwa, mwanafunzi aingie katika tovuti ya NACTVET (www.nactvet.go.tz), kisha ajiridhishe kuwa amesajiliwa kwa kuhakiki taarifa zake kwa kubonyeza “link” inayosomeka “student’s information verification”.

Mambo ya Kuzingatia kwa Wanaoomba Moja kwa Moja Vyuoni:

  1. Muombaji anaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja. Kuchaguliwa katika chuo alichoomba kutategemea ushindani utakaokuwepo katika chuo hicho.
  2. Muombaji akishachaguliwa na chuo, chuo husika kitawasilisha taarifa za muombaji NACTVET kwa ajili ya uhakiki. Muombaji atapokea ujumbe ukimtaarifu kuwa taarifa zake zimewasilishwa NACTVET na chuo kwa ajili ya kuhakikwa
  3. Baada ya taarifa zake kuhakikiwa, atapokea ujumbe kutoka NACTVET ukimjulisha kuwa amehakikwa, na utakuwa na msimbo (code) ambao atatakiwa kuutumia kuangalia taarifa zake za uhakiki. Pia atatakiwa kuutunza msimbo huo na kuuwasilisha kwa chuo alichochaguliwa siku atakapokwenda katika chuo hicho kwa ajili ya kuanza masomo.
  4. Baada ya kuwasilisha msimbo huo chuoni, atasajiliwa na chuo, kisha atapokea ujumbe kutoka NACTVET ukimueleza kuwa amesajiliwa.
  • Baada ya kusajiliwa, mwanafunzi anatakiwa aingie katika tovuti ya NACTVET (www.nactvet.go.tz), kisha ajiridhishe kuwa amesajiliwa kwa kuhakiki taarifa zake kwa kubonyeza “link” inayosomeka “student’s information verification”.
Buy JNews Buy JNews Buy JNews
ADVERTISEMENT

Usikose Kusoma na Hizi Pia

Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Uhakiki NACTE Online (NACTE Student Verification Results Online)

Kozi ya Ordinary Diploma in Environmental Management, Sifa na Vigezo, Vyuo Vinavyotoa

Kozi ya Ordinary Diploma in Social Work, Sifa na Vigezo, Vyuo Vinavyotoa

Kozi ya Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences, Sifa na Vigezo, Vyuo Vinavyotoa

Load More
SendShareShareTweet
Zoteforum

Zoteforum

Karibu Zoteforum.com, Tovuti yako pekee inayokupasha habari na Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani.

Makala Nyingine zaidi

Chuo cha Arusha Technical College: Kozi Zinazotolewa, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga

Chuo cha Excellent College of Health and Allied Sciences – Kibaha: Kozi zinazotolewa, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga na Chuo

July 5, 2025
Chuo cha Arusha Technical College: Kozi Zinazotolewa, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga

Chuo cha Elijerry College of Health and Allied Sciences: Kozi zinazotolewa, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga

July 5, 2025

Chuo cha City College of Health and Allied Sciences – Mwanza Campus: Kozi, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga

June 10, 2025

Chuo cha Arusha Technical College: Kozi Zinazotolewa, Maombi ya Udahili, Ada za Masomo, na Fomu za Kujiunga

June 10, 2025

Mwongozo wa Udahili: NACTE Admission Guidebook 2025/26 Pdf

June 1, 2025

Ada Na Kozi Zinazotolewa Na Chuo Cha Kizumbi Institute of Cooperative Business Education (KICoB) (KICoB Courses And Fees)

April 16, 2025
Load More

Weka maoni yako hapa au Komenti kuhusu makala hiiCancel reply

Recommended Stories

Fahamu ugonjwa wa Vitiligo, Sababu, Dalili zake na Tiba

Dalili za ugonjwa wa Vitiligo, Sababu na Tiba

April 27, 2025
Zifahamu shule zote za Sekondari zilizopo katika Wilaya Ya Mtama

Orodha Ya Shule Za Sekondari Wilaya Ya Mtama

May 6, 2025
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Udahili wa Chuo Kikuu cha Kairuki kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026 (KU Application 2025/2026)

Maombi ya Udahili Chuo Kikuu cha Kairuki(KU Application 2025/2026)

April 18, 2025
Sifa Za Kujiunga Na Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara University College (STeMMUCo) 2025/2026

Sifa Za Kujiunga Na Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara University College (STeMMUCo) 2025/2026

April 17, 2025
Zuchu – Antenna mp3 download

Zuchu – Antenna mp3 download

November 13, 2024
Matokeo ya Darasa la Saba 2024 (NECTA PSLE Results)

Matokeo ya Darasa la Saba 2024 Tanga

October 29, 2024
Maombi ya Udahili Chuo Kikuu cha Institute of Accountancy Arusha(IAA Application )

Maombi ya Udahili Chuo Kikuu cha Institute of Accountancy Arusha(IAA Application 2025/2026)

April 18, 2025
Majina Ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha TEKU

Majina Ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha TEKU 2025/2026 (TEKU Selected Applicants pdf)

April 19, 2025
Zifahamu Shule Zote za Sekondari Zilizopo Katika Wilaya Ya Nanyumbu, Matokeo ya NECTA na Mock, Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza na cha Tano, na Utaratibu wa Kujiunga na Masomo Katika Shule Hizo

Orodha Ya Shule Za Sekondari Wilaya Ya Nanyumbu, Matokeo, Majina ya Waliochaguliwa na Utaratibu wa Kujiunga na Masomo

May 11, 2025
  • About
  • Cart
  • Checkout
  • Contact
  • Download Mziki na Nyimbo mpya
  • Habari za Burudani
  • Habari za Elimu
  • Habari za Soka
  • Home
  • Matokeo Ya Mitihani Tanzania – NECTA – MOCK – VYUO
  • My account
  • Nafasi za Kazi 2024
  • Offerings
  • Shop
  • Subscription
Call us: +1 234 JEG THEME

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.