zoteforum.com
No Result
View All Result
  • Login
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
PRICING
JIUNGE
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
No Result
View All Result
zoteforum.com
No Result
View All Result

Nafasi Za Ajira Za Mikataba Kwa Kada Za Afya (ajira 400)

Tangazo La Nafasi Za Ajira Za Mikataba Kwa Kada Za Afya

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya inaendelea na utekelezaji wa mpango wa uwekezaji katika afya ya mama na mtoto nchini Tanzania yaani Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na  Serikali  za  Mitaa  inawatangazia wananchi wote raia wa Tanzania wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi za ajira za 400 za Mkataba  kwa Kada za Afya watakaofanya kazi katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Hivyo, wahitimu kutoka kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu na Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kuanzia tarehe 6 – 20, Desemba, 2024. Nafasi za ajira zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).

1 TARATIBU ZA KUOMBA AJIRA ZA MKATABA KWA KADA ZA AFYA

Wataalamu wa Kada za Afya wenye sifa wanatakiwa kufuata utaratibu ule ule  wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Waombaji waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa  kuhuisha taarifa zao na barua za maombi. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

ADVERTISEMENT

Sifa za Kitaaluma za Waombaji wa Kada za Afya

2 Daktari Daraja la II – TGHS E

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

  • Shahada ya udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja;
  • Usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika); na
  • Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

3 Tabibu Meno Daraja la II – TGHS B

Waombaji wanatakuwa kuwa na,

  • Stashahada ya Tabibu Meno (Diploma in Clinical Dentistry/NTA level 6) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali;
  • Usajili     kutoka  Baraza  la           Madaktari        Tanganyika              (Medical            Council   of Tanganyika); na
  • Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

4 Tabibu Daraja la II – TGHS B

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

  • Stashahada ya Utabibu (Diploma in Clinical Medicine) ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali; na
  • Leseni hai kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

5 Mteknolojia (Dawa) Daraja la II TGHS – B

Waombaji wanatakiwa wawe Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika fani ya Dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wafamasia.

6 Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II TGHS – B

Waombaji wanatakiwa kuwa na,

  • Stashahada ya Uuguzi (Diploma) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council); na
  • Leseni hai kutoka Baraza la Uuuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

7 Mteknolojia Msaidizi Maabara – TGHS A

  • Waombaji wawe na Astashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Certificate in Health Laboratory Science) kwa muda wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
  • Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

8 Mteknolojia (Mionzi) Daraja la II TGHS – B

  • Wahitimu wa Stashahada katika fani ya Mionzi (Diploma in Radiology/Radiography/NTA leve 6) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
  • Wenye usajili kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging Professionals Council); na
  • Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Mionzi Tanzania (The Medical Radiology and Imaging Professionals Council).

9 Mteknolojia (Maabara) Daraja Ii

  • Waombaji wawe na Stashahada katika fani ya Uteknolojia wa Maabara ya Afya (Diploma in Health Laboratory Sciences) kwa muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).
  • Wenye Leseni hai kutoka Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya (Health Laboratory Practitioners’ Council).

10 Muuguzi Daraja La Ii

  • Waombaji wawe na cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).
    • Wawe na Leseni hai kutoka Baraza la Uuuguzi na Ukunga Tanzania (Tanzania Nurse and Midwifery Council).

11 Mteknolojia Msaidizi (Dawa)

Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha miaka miwili katika    fani ya teknolojia ya dawa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Baraza lao la Taaluma.

12 MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:

  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 45;
  • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika);
  • Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini  ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
  • Kwa waombaji waliosajiliwa na mabaraza ya taaluma ni lazima awe na Leseni hai kutoka Baraza la taaluma yake
  • Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika  Utumishi  wa  Umma;
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
  • Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

13 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE

  • Waombaji wote  wawe  tayari  kufanya  kazi  katika  Halmashauri  yeyote watakayopangiwa
    • Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha nyaraka zote muhimu kwenye mfumo; na
  • Maombi ya ajira hizi ni bure.

WAHITIMU WALIOSOMA NJE YA NCHI

  • Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi  wanatakiwa  kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ…
  • kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ili kuwawezesha kuingia kwenye Mfumo wa Ajira; na
  • Waombaji waliosoma Vyuo vya Nje ya Nchi wanatakiwa kupata Ithibati ya masomo yao kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) ili vyeti vyao viweze kutambuliwa na kupata uhalali wa kutumika hapa nchini.

Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au wasiliana na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210 kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.

Waombaji wenye Ulemavu na sifa zilizoainishwa katika tangazo hili  watume maombi yao pia kupitia mfumo. Aidha, maombi yao yaeleze aina ya ulemavu alionao na kuambatisha picha na taarifa ya uthibitisho wa Daktari kutoka katika hospitali za  Serikali.

Maombi yeyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja Ofisi ya Rais – TAMISEMI hayatafanyiwa kazi.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20 Desemba, 2024 saa 05:59  usiku. Tangazo hili linapatikana katika tovuti zifuatazo: www.tamisemi.go.tz

Limetolewa na:                

Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais – TAMISEMI,

Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P 1923,

41185 DODOMA.

06 Desemba ,2024.

PAKUA PDF YA TANGAZO HILI HAPA

Usikose Kusoma na Hizi Pia

VITUO VYA USAILI WA MAHOJANO WA MDAs & LGAs UTAKAOFANYIKA TAREHE 22 HADI 24 OKTOBA, 2025

Serikali yatangaza Nafasi za Kazi za ualimu (10,026)

Nafasi za kazi Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II)

Nafasi za kazi Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daro la II

Nafasi za kazi MSANIFU MAJENGO DARAJA LA II (ARCHITECT GRADE II)

Nafasi za kazi Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Daraja la II (Aquaculture Officer Grade II)

Nafasi za kazi FUNDI SANIFU DARAJA LA II – KILIMO (AGRICULTURAL TECHNICIAN GRADE II)

Nafasi za kazi Mkufunzi DARAJA LA II – Kilimo (Agricultural Officer Grade II)

Nafasi za kazi Afisa Kilimo Msaidizi DARAJA LA III (Agricultural Field Officers)

Nafasi za kazi Afisa Kilimo Msaidizi DARAJA LA II (Agricultural Field Officers)

Load More
SendShareShareTweet
Zoteforum

Zoteforum

Karibu Zoteforum.com, Tovuti yako pekee inayokupasha habari na Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani.

Makala Nyingine zaidi

VITUO VYA USAILI WA MAHOJANO WA MDAs & LGAs UTAKAOFANYIKA TAREHE 22 HADI 24 OKTOBA, 2025

VITUO VYA USAILI WA MAHOJANO WA MDAs & LGAs UTAKAOFANYIKA TAREHE 22 HADI 24 OKTOBA, 2025

Serikali yatangaza Nafasi za Kazi za ualimu (10,026)

Serikali yatangaza Nafasi za Kazi za ualimu (10,026)

Nafasi za kazi Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II)

Nafasi za kazi Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daro la II

Nafasi za kazi MSANIFU MAJENGO DARAJA LA II (ARCHITECT GRADE II)

Nafasi za kazi Afisa Ukuzaji Viumbe Kwenye Maji Daraja la II (Aquaculture Officer Grade II)

Load More

Weka maoni yako hapa au Komenti kuhusu makala hiiCancel reply

  • About
  • Cart
  • Checkout
  • Contact
  • Download Mziki na Nyimbo mpya
  • Habari za Burudani
  • Habari za Elimu
  • Habari za Soka
  • Home
  • Matokeo Ya Mitihani Tanzania – NECTA – MOCK – VYUO
  • My account
  • Nafasi za Kazi 2024
  • Offerings
  • Shop
  • Subscription
Call us: +1 234 JEG THEME

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.