zoteforum.com
No Result
View All Result
  • Login
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
PRICING
JIUNGE
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa
No Result
View All Result
zoteforum.com
No Result
View All Result

NAFASI ZA KAZI (15) HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU 01-08-2025


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuomba nafasi za kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali kwa mwaka wa fedha 2023/2024, chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024, na kibali chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.228/01C/021 cha tarehe 20/05/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 12

1.1 KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaidana za siri; ii. Kupokea wageni na kuwa sikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa; iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine; iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi; v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemuhusika; vi. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika; vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na ix. Kufanyakazi zingine utakazopangiwa na Mkuu wako wa kazi.

1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe na Elimu ya kidato cha nne au kidato cha sita mwenye Stashahada ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
  • Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja.
  • Apate programu za kompyuta za Ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Email na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C kwa mwezi.


2.0 DEREVA DARAJA II – NAFASI 3

2.1 MAJUKUMU YA KAZI YA DEREVA II

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari; ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi; iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari; iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote; v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; vi. Kufanya usafi wa gari; vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

2.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe amehitimu Kidato cha nne (Form IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha nne (IV).
  • Awe na Leseni ya Daraja la ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji magari.
  • Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali.
  • Awe na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.1.2 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi.


MASHARTI YA JUMLA YA MWOMBAJI KAZI

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45;

ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha katika mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao; iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili;

Usikose Kusoma na Hizi Pia

SUA Selected Applicants 2025/2026 pdf (Majina Ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha SUA )

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Dodoma

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mwanza

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Katavi

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Kagera

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Iringa

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Geita

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Kilimanjaro

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Dar es Salaam

Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Arusha

Load More
Buy JNews Buy JNews Buy JNews
ADVERTISEMENT

iv. Waombaji ambao tayari ni Waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CCA. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010;

v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika;

vii. Testimonies, Provisional Results, Statements of Results, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA;

viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE);

ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi; x. Waombaji wenye majina tofauti katika vyeti vya taaluma, kuzaliwa na NIDA waambatishe DEED POLL (Hati ya usajili wa kiapo cha Majina);

xi. Waombaji ambao wana utofauti wa herufi katika kitambulisho cha Taifa na vyeti vya taaluma, kidato cha sita, kidato cha nne na cheti cha kuzaliwa wanatakiwa kuambatisha AFFIDAVIT (Kiapo);

xii. Waombaji wa kazi ya Dereva Daraja II wenye Leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo vya udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika;

xiii. Waombaji watakao wasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria;

xiv. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 14/08/2025.


MUHIMU:

  • Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
  • Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, S.L.P 97, Kasulu.
  • Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na: CPA Francis G. Kafuku MKURUGENZI MTENDAJI (W) HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU

DOWNLOAD TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU 01-08-2025

SendShareShareTweet
Zoteforum

Zoteforum

Karibu Zoteforum.com, Tovuti yako pekee inayokupasha habari na Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani.

Makala Nyingine zaidi

NAFASI ZA KAZI 6 – Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NANYUMBU 02-08-2025

NAFASI ZA KAZI 6 – Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

WALIOITWA KAZINI CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI 01-08-2025

WALIOITWA KAZINI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 01-08-2025

TANGAZO LA KUITWA KAZINI KITUO CHA ZANA ZA KILIMO NA TEKNOLOJIA VIJIJINI (CAMARTEC) 01-08-2025

NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA KIGOMA UJIJI 01-08-2025

NAFASI ZA KAZI (7)HALMASHAURI YA MJI WA BABATI 01-08-2025

Load More

Weka maoni yako hapa au Komenti kuhusu makala hiiCancel reply

  • About
  • Cart
  • Checkout
  • Contact
  • Download Mziki na Nyimbo mpya
  • Habari za Burudani
  • Habari za Elimu
  • Habari za Soka
  • Home
  • Matokeo Ya Mitihani Tanzania – NECTA – MOCK – VYUO
  • My account
  • Nafasi za Kazi 2024
  • Offerings
  • Shop
  • Subscription
Call us: +1 234 JEG THEME

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In
No Result
View All Result
  • Home
  • Nafasi za kazi
  • Elimu
    • HESLB
    • Orodha ya Shule za sekondari Tanzania
    • selections
      • Majina Ya Waliochaguliwa Vyuo vikuu
    • NECTA Matokeo
    • Maombi ya Udahili
      • Sifa za Kujiunga na Vyuo
      • Kozi za Vyuo
      • Orodha ya Vyuo
  • Internship
  • Habari na Matukio
    • Afya
    • Tekinolojia
  • Burudani
    • Soka
    • Mziki
    • Mapenzi na Mahusiano
  • Biashara
    • Magari
    • bei za bidhaa

© 2024 Zoteforum - Tovuti yako pekee inayokusogezea Makala mpya kuhusu elimu, michezo, na burudani. by Zoteforum.com.