TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Utangulizi
Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Babati anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo:
1. Nafasi za Kazi
1.1 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi Tatu (03)
1.1.1 Majukumu ya Kazi
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri ii. Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa. iii. Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine. iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi. v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/sehemu husika. vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika. vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali. viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
1.1.2 Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa awe na Elimu ya Kidato cha Nne au Sita, wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programme za kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.3 Mshahara
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C.
1.2 Dereva Daraja la II – Nafasi Nne (04)
1.2.1 Majukumu ya Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari. ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi. iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari. iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote. v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali. vi. Kufanya usafi wa gari. vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
1.2.2 Sifa za Mwombaji
Waombaji wawe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.3 Ngazi ya Mshahara
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ni TGS B.
2. Masharti ya Jumla
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (Email Address) pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificate – Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne na cha Sita, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
v. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, hatiza matokeo za Kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWI KUENDELEA NA USAILI.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa kuambatisha vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Waombaji watakaowasilisha taarifa na sifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 Agosti, 2025.
xiii. Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”).
xiv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKILIWA.
3. Msimamizi wa Ajira
MKURUGENZI WA MJI S.L.P 383 BABATI
4. Tamko la Mwisho
Imetolewa na: MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA BABATI
KUJUA ZAIDI PAKUA