Tangazo la kazi ya Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daro la II
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 7 za Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daro la II kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kufundisha fani mbalimbali za michezo katika eneo lake la kazi. ii. Kukusanya takwimu mbalimbali za sekta ya michezo katika eneo lake la kazi. iii. Kusaidia kutambua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa watoto katika eneo lake la kazi. iv. Kushauri namna ya uendeshaji wa vyama na vilabu vya michezo katika eneo lake la kazi kwa kuzingatia taratibu zilizopo. v. Kusaidia kuendeleza fani ya michezo ya jadi katika eneo lake la kazi. vi. Kushauri kuhusu uendeshaji wa miundombinu ya michezo katika eneo lake la kazi. vii. Kusaidia kuhamasisha michezo kwa wote katika eneo lake la kazi.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Astashada ya Elimu ya Michezo (Physical Education), sayansi ya michezo (certificate in sports science), uongozi na utawala wa michezo (sports management and administration), Elimu ya michezo (Sports coaching and Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
14.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS. B
KUTUMA MAOMBI YAKO BOFYA HAPA
MASHARTI YA JUMLA NA JINSI YA KUTUMA MAOMBI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate.
- “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.