Tangazo la kazi ya Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II)
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 5 za Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
15.1 Majukumu ya Kazi
i. Kusimamia manzuki; ii. Kutunza hifadhi za nyuki, iii. Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki, iv. Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti, v. Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo, vi. Kutoa leseni za biashara za mazao ya nyuki, vii. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki, viii. Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.
15.2 Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Ufugaji Nyuki kutoka Vyuo vinavotambuliwa na Serikali.
15.3 Ngazi ya Mshahara
TGS.C
KUTUMA MAOMBI YAKO BOFYA HAPA
MASHARTI YA JUMLA NA JINSI YA KUTUMA MAOMBI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.