TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 17710 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MDAs NA LGAs 16-10-2025
NAFASI HIZO NI KAMA IFUATAVYO
- Mhasibu Daraja la II (Accountant Grade II) – Nafasi 131
- Afisa Ukuaji Viumbe Kwenye Maji Msaidizi Daraja la II (Assistant Aquaculture Officer Grade II) – Nafasi 1
- Msaidizi wa Hesabu Daraja la II (Accounts Assistant Grade II) – Nafasi 126
- Afisa Tawala Daraja la II (Administrative Officer Grade II) – Nafasi 32
- Afisa Hesabu Daraja la II (Accounts Officer II) – Nafasi 224
- Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agro Engineers) – Nafasi 24
- Afisa Uvuvi Msaidizi Daraja la II (Assistant Fisheries Officer II) – Nafasi 35
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la II (Agricultural Field Officers) – Nafasi 292
- Afisa Kilimo Msaidizi Daraja la III (Agricultural Field Officers) – Nafasi 76
- Mkufunzi Daraja la II-Kilimo (Agricultural Officer Grade II) – Nafasi 73
- Fundi Sanifu Daraja la II-Kilimo (Agricultural Technician Grade II) – Nafasi 15
- Afisa Ukuaji Viumbe Kwenye Maji Daraja la II (Aquaculture Officer Grade II) – Nafasi 3
- Msanifu Majengo Daraja la II (Architect Grade II) – Nafasi 62
- Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II (Assistant Game and Sports Development Officer Grade II) – Nafasi 7
- Afisa Ufugaji Nyuki Msaidizi Daraja la II (Assistant Beekeeping Officer II) – Nafasi 5
- Afisa Mlezi wa Watoto Msaidizi Daraja la II (Assistant Child Care Officer Grade II) – Nafasi 5
- Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Community Development Officer II) – Nafasi 179
- Afisa Utamaduni Msaidizi (Assistant Cultural Officer Grade) – Nafasi 1
- Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II (Assistant Environmental Health Officer Grade II) – Nafasi 161
- Afisa TEHAMA Msaidizi Daraja la II (Assistant ICT Officer Grade II) – Nafasi 35
- Afisa Muuguzi Msaidizi II (Assistant Nursing Officer Grade II) – Nafasi 3945
- Afisa Ununuzi Msaidizi Daraja la II (Assistant Procurement Officer Grade II) – Nafasi 16
- Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi Daraja la II (Assistant Social Welfare Officer Grade II) – Nafasi 76
- Afisa Ugavi Msaidizi Daraja la II (Assistant Supplies Officer Grade II) – Nafasi 18
- Msaidizi wa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Assistant Grade II) – Nafasi 6
- Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Officer Grade II) – Nafasi 21
- Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineer Grade II) – Nafasi 17
- Fundi Sanifu Vifaa Tiba Daraja la II (Biomedical Engineering Technician Grade II) – Nafasi 34
- Mhandisi Ujenzi Daraja la II (Civil Engineer Grade II) – Nafasi 53
- Fundi Sanifu Msaidizi Ujenzi Daraja la II (Civil Technician Grade II) – Nafasi 48
- Mpishi Daraja la II (Cook Grade II) – Nafasi 1127
- Katibu wa Kamati Daraja la II (Committee Clerk Grade II) – Nafasi 43
- Afisa Maendeleo ya Jamii Daraja II (Community Development Officer Grade II) – Nafasi 43
- Mpishi Daraja la II (Cook II) – Nafasi 43
- Afisa Ushirika Daraja la II (Cooperative Officer Grade II) – Nafasi 45
- Afisa Mifugo Msaidizi Daraja la II (Livestock Field Officer Grade II) – Nafasi 252
- Afisa Utamaduni Daraja la II (Cultural Officer Grade II) – Nafasi 38
- Daktari wa Upasuaji wa Kinywa na Meno II (Dental Surgeon Grade II) – Nafasi 68
- Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II (Dental Therapist Grade II) – Nafasi 217
- Dereva Daraja la II (Driver Grade II) – Nafasi 427
- Mchumi Daraja la II (Economist Grade II) – Nafasi 138
- Afisa wa Sheria Daraja la II (Legal Officer Grade II) – Nafasi 140
- Afisa Muuguzi Daraja la II (Nursing Officer Grade II) – Nafasi 712
- Afisa Mifugo Daraja la II (Livestock Officer Grade II) – Nafasi 59
- Afisa Mifugo Msaidizi Daraja la III (Livestock Field Officer Grade III) – Nafasi 15
- Afisa Afya Mazingira Daraja la II (Environmental Health Officer Grade II) – Nafasi 96
- Mhandisi II Mazingira (Environmental Engineer Grade II) – Nafasi 4
- Afisa Mazingira Daraja la II (Environmental Officer Grade II) – Nafasi 90
- Afisa Uvuvi Daraja la II (Fisheries Officer Grade II) – Nafasi 55
- Afisa Misitu Daraja la II (Forest Officers Grade II) – Nafasi 46
- Fiziotherapia Daraja la II (Physiotherapist Grade II) – Nafasi 43
- Afisa Wanyamapori Daraja la II (Game Officer Grade II) – Nafasi 32
- Mhifadhi Wanyamapori Daraja la II (Game Warden Grade II) – Nafasi 16
- Mhifadhi Wanyamapori Daraja la III (Game Warden Grade III) – Nafasi 2
- Afisa Mipango Daraja la II (Planning Officer Grade II) – Nafasi 90
- Afisa Michezo Daraja la II (Games and Sports Development Officer Grade II) – Nafasi 42
- Mjiolojia Daraja la II (Geologist Grade II) – Nafasi 9
- Msaidizi wa Afya Daraja la II (Health Assistant Grade II) – Nafasi 1588
- Afisa Mteknolojia Daraja la II – Maabara (Health Laboratory Scientists Grade II) – Nafasi 33
- Katibu wa Afya Daraja la II (Health Secretary Grade II) – Nafasi 32
- Afisa Rasilimali Watu Daraja la II (Human Resource Officer Grade II) – Nafasi 21
- Afisa Habari Daraja la II (Information Officer Grade II) – Nafasi 84
- Afisa Ukaguzi wa Ndani Daraja la II (Internal Audit Officer Grade II) – Nafasi 75
- Mkaguzi wa Ndani Daraja II (Internal Auditor Grade II) – Nafasi 102
- Mteknolojia Maabara II (Health Laboratory Technologist Grade II) – Nafasi 30
- Dobi Daraja la II (Launderer Grade II) – Nafasi 10
- Afisa Mipango Miji Daraja la II (Town Planner Grade II) – Nafasi 86
- Fundi Sanifu Daraja la II (Mechanical Technician Grade II) – Nafasi 12
- Daktari Daraja la II (Medical Officer Grade II) – Nafasi 1201
- Afisa Lishe Daraja la II (Nutrition Officer Grade II) – Nafasi 57
- Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II (Occupational Therapist Grade II) – Nafasi 12
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary Grade II) – Nafasi 308
- Mfamasia Daraja la II (Pharmacist Grade II) – Nafasi 138
- Afisa Ununuzi Daraja la II (Procurement Officer Grade II) – Nafasi 114
- Mkaguzi wa Ndani Daraja II (Internal Auditor Grade II) – Nafasi 97
- Msaidizi wa Kumbukumbu (Nyaraka) Daraja la II (Records Management Assistant Grade II) – Nafasi 239
- Afisa Kumbukumbu Daraja la II (Records Officer Grade II) – Nafasi 29
- Fundi Sanifu Maabara ya Shule Daraja la II (School Laboratory Technician Grade II) – Nafasi 90
- Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II (Social Welfare Officer Grade II) – Nafasi 148
- Mtakwimu Daraja la II (Statistician Grade II) – Nafasi 100
- Afisa Ugavi Daraja la II (Supplies Officer Grade II) – Nafasi 76
- Afisa Utalii Daraja la II (Tourism Officer Grade II) – Nafasi 16
- Afisa Biashara Daraja la II (Trade Officer Grade II) – Nafasi 164
- Afisa Usafirishaji Daraja la II (Transport Officer Grade II) – Nafasi 51
- Daktari wa Mifugo Daraja la II (Veterinary Officers Grade II) – Nafasi 36
- Mteknolojia Dawa Daraja II (Technologist Pharmacy Grade II) – Nafasi 130
- Mwalimu Daraja la IIIA (Teacher Grade IIIA) – Nafasi 3018
KUPAKUA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MDAs NA LGAs 16-10-2025 BOFYA HAPA TANGAZO_LA_NAFASI_ZA_KAZI__ZA_MDAs_&_LGAs[1]Download
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa wale walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuwasilisha maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu walionao kwenye mfumo wa kuomba ajira kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria au Wakili.
- Waombaji walioajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE, na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo na nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria au Wakili ikiwa ni pamoja na:
- Vyeti vya kuzaliwa,
- Vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho,
- Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali (Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates),
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI,
- Vyeti vya computer,
- Vyeti vya kitaaluma kutoka kwa bodi husika.
- “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, na hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Form IV and Form VI results slips) HAZITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA na NACTE.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa au sifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu viambatishwe na anuani ya barua ielekezwe kwa: KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, S. L. P. 2320, Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwenye sehemu ya ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayatafikirwa.
Limelindwa na: KATIBU, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
ADVERTISEMENT
Nafasi za fundi bomba mbona hakuna